` CRDB YAKABIDHI MABANGO KUHAMASISHA UTUNZAJI MAZINGIRA KAHAMA

CRDB YAKABIDHI MABANGO KUHAMASISHA UTUNZAJI MAZINGIRA KAHAMA

Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana (kulia) akikabidhi sehemu ya mabango ya kuhamasisha utunzaji mazingira kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Stephen Magalla 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog

Benki ya CRDB imekabidhi mabango 21 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa ajili ya kuhamasisha usafi na utunzaji mazingira katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo leo Alhamisi, Septemba 18, 2025, Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana, amesema benki hiyo imejipanga kuunga mkono juhudi za serikali na jamii katika kupendezesha miji na kulinda mazingira.

“Benki ya CRDB tupo bega kwa bega na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kupitia kampeni ya 'Kahama Kwa Pamoja - Usafi Daima' – kwenye bango haya kuna ujumbe kama 'Tunza Mazingira Yakutunze, Usitupe Taka Ovyo’. Kupitia mabango haya tunalenga kuelimisha wananchi kuimarisha usafi na utunzaji mazingira,” amesema Wagana.

Ameongeza kuwa benki hiyo pia itatoa miche ya miti kwa ajili ya kupandwa pindi mvua zitakapoanza, lengo likiwa ni kuifanya Kahama kuwa mji safi, ya kijani na rafiki kwa mazingira.

Kwa upande wake, Meneja wa CRDB Kahama Social, Bahini Martine Mitundwa, amesema Kahama ni lango kuu la biashara hivyo benki hiyo imeona umuhimu wa kuwekeza kwenye kampeni za mazingira ili kulinda hadhi na mvuto wa mji huo.

Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Utunzaji Mazingira Manispaa ya Kahama, Johannes Mwebe, amewataka wananchi kushirikiana kwa vitendo kwa kuepuka kutupa taka hovyo na kushiriki kupanda miti.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Stephen Magalla, ameishukuru CRDB kwa mchango wake, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni chachu kubwa ya kuimarisha kampeni za usafi na afya ya jamii.

“Ili tuwe salama kiafya ni lazima mazingira yetu yawe safi. Tukidumisha usafi, tunajiepusha na magonjwa. Hivyo basi nawasihi wananchi wote kutambua kuwa jukumu la kulinda mazingira ni la kila mmoja wetu – Kahama kwa Pamoja - Usafi Daima,” amesema Magalla.
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana (kulia) akikabidhi sehemu ya mabango ya kuhamasisha utunzaji mazingira kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Stephen Magalla. Picha na Kadama Malunde 
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana (kulia) akikabidhi sehemu ya mabango ya kuhamasisha utunzaji mazingira kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Stephen Magalla 
Sehemu ya mabango ya kuhamasisha utunzaji mazingira yaliyotolewa na Benki ya CRDB
Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati akikabidhi mabango ya kuhamasisha utunzaji mazingira katika Manispaa ya Kahama

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Stephen Magalla akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi mabango ya kuhamasisha utunzaji mazingira katika Manispaa ya Kahama.

Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Utunzaji Mazingira Manispaa ya Kahama, Johannes Mwebe akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi mabango ya kuhamasisha utunzaji mazingira katika Manispaa ya Kahama.
Meneja wa CRDB Kahama Social, Bahini Martine Mitundwa akizungumza wakati Benki ya CRDB ikikabidhi mabango ya kuhamasisha utunzaji mazingira katika Manispaa ya Kahama.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464