` HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA YATOA MIKOPO YA SH.MILIONI 299.4 KWA VIKUNDI VYA VIJANA NA WANAWAKE

HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA YATOA MIKOPO YA SH.MILIONI 299.4 KWA VIKUNDI VYA VIJANA NA WANAWAKE

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imetoa mikopo yenye thamani ya Sh. milioni 299.4 kwa vikundi 26 vya wanawake na vijana, ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi.

Hafla ya utoaji wa mikopo hiyo imefanyika leo septemba 18,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ambapo wanufaika walipewa kwamnza mafunzo ya matumizi sahihi ya fedha hizo ili zitekeleze malengo yaliyokusudiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Dk.Kalekwa Kasanga,amesema utoaji wa mikopo hiyo ni awamu ya tatu sasa, ambapo awamu ya kwanza walitoa sh.milioni 152,5 awamu ya pili sh,milioni 537.8 na sasa awamu ya tatu wanatoa tena sh.milioni 299.4 kwa vikundi 26, ambapo vijana vikundi 12 na wanawake vikundi 14.

“Nawaomba wanufaika wote wa mikopo hii mzitumie fedha hizi kwa malengo kusudiwa na siyo vinginevyo, ili zipate kuwa kwamua kiuchumi, na vijana msiende kuzichezea Kamari na wanawake kununua vitenge,”amesema Dk.Kalekwa.
Kwa upande wake, mgeni rasmi katika hafla hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga, aliwataka wanufaika kutumia fedha hizo vizuri ili wainuke kiuchumi, pamoja na kusimamia mipango yao na siyo fedha hizo kuzibadilishia matumizi.

Pia,amesisitiza urejeshaji wa mikopo kwa wakati,huku akiwaagiza Watendaji wa Kata kuhakikisha wanakuwa karibu na vikundi hivyo,hivi ili kubaini changamoto ambazo zitawakabili na kuwasaidia wasikwame kwenye uendeshaji wa miradi yao ya kiuchumi.

Baadhi ya wanufaika akiwemo Mariam Mjema, wamesema mikopo hiyo itakuwa mkombozi wao kiuchumi, huku wakiahidi kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Kalekwa Kasanga,akizungumza kwenye hafla hiyo.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mfano wa hundi ya fedha ya mikopo sh.milioni 299.4 ikitolewa kwa vikundi 26 vya wanawake na vijana halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Joseph Ntomela akizungumza kwenye hafla hiyo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464