` RC MBONI APOKEA VIKOMBE VIWILI KUTOKA KWA TIMU YA RS SHINYANGA SPORT CLUB BAADA YA KUPATA USHINDI MASHINDANO YA SHIMIWI

RC MBONI APOKEA VIKOMBE VIWILI KUTOKA KWA TIMU YA RS SHINYANGA SPORT CLUB BAADA YA KUPATA USHINDI MASHINDANO YA SHIMIWI


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe Mboni Mhita,amepokea vikombe viwili vilivyoshindwa na Timu ya RS Shinyanga Sport Club katika mashindano ya 39 ya Shirikisho la Michezo la Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Tawala za Mikoa (Shimiwi).
Makamu Mwenyekiti wa RS Shinyanga Sport Club Wiliam Masala,akizungumza leo Septemba 17,2025 kabla ya kumkabidhi vikombe viwili Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita,ambavyo wameshinda kwenye mashindano hayo ya Shimiwi,amesema timu yao ilikuwa na watu 15 na walishiriki michezo nane.

Amesema katika michezo hiyo walioifanya kwa ufanisi ni mbio za kupokezana vijiti, kurusha vishale, huku mchezo wa karata wakiimbuka mabingwa wa kitaifa kwa upande wa wanaume, na kwa wanawake wameibuka washindi wa tatu kitaifa.
“Vikombe ambavyo tumeshinda na kumkabidhii Mkuu wa Mkoa leo, ni kikombe cha ubingwa kitaifa kwa upande wa mchezo wa karata, na kikombe cha pili,ni cha ubingwa mshindi wa tatu kwa upande wa wanawake mchezo huo huo wa Karata,”amesema Masala.

Amesema, Mashindano hayo yalianza kufanyika kuanzia Septemba 1 hadi 16,2025 na yalifanyika Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita,ameipongeza Timu hiyo kwa kuibuka washindi kwenye baadhi ya michezo na kuja na vikombe viwili,na kwamba wataendelea kuwa nao pamoja kwa kila hatua.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni, amepongeza ushindi huo, na kwamba watumishi hao wameuheshimisha mkoa kwa kurudi na vikombe viwili.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita,akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa vikombe viwili mashindano ya Shimiwi.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni akizungumza kwenye hafla hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa RS Shinyanga Sport Club Wiliam Masala akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita (kulia)akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni akiwa wamebeba makombe mawili ya ushindi mashindano ya Shimiwi.






Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464