` KATAMBI AUNGURUMA KOLANDOTO AMUOMBEA KURA RAIS SAMIA

KATAMBI AUNGURUMA KOLANDOTO AMUOMBEA KURA RAIS SAMIA

KATAMBI AUNGURUMA KOLANDOTO AMUOMBEA KURA RAIS SAMIA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi amefanya mkutano wa kampeni Kata ya Kolandoto na kunadi sera na ilani ya CCM,huku akimuombea kura nyingi za ndiyo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan siku ya uchaguzi Mkuu Oktoba 29.

Mkutano huo umefanyika leo Septemba 17,2025 na kuhudhuliwa na wananchi na wana CCM na Wabunge wateule wa Vitimaalum.
Katambi akinadi sera kwenye mkutano huo,amesema yeye kampeni zake ni za kuwaeleza wananchi wamewafanyia nini ndani ya kipindi cha miaka iliyopita, na atafanya nini endapo wananchi wakimpatia ridhaa ya kuwa Mbunge wao tena.

Amesema, Katika Kata ya Kolandoto kwa upande wa sekta ya Afya amejenga Zahanati ikiwamo ya Gharama,Mwamagunguli na Mwanumbi na kwamba akipata tena ridhaa zitajengwa Zahanati nyingi mpya 5 katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga.
Amesema,kipindi kilichipo pia ameshajenga Zahanati Mpya 5 na ataendelea kujenga zingine ili kuhakikisha huduma za afya zinafika karibu na wananchi, pamoja na kujenga vituo vya afya na upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa.

Amesema katika Kata hiyo ya Kolandoto, pia atakipandisha hadhi Chuo cha Sayansi za Afya,ili kiwe Chuo kikuu,pamoja na kujenga Barabara ya kwenda Hospitali ya Kolandoto kwa kiwango cha Lami.
Amesema kwa upande wa Elimu amejenga shule mpya ya msingi Mwanasanae, pamoja na Madarasa 12, na kwamba pia watajenga madarasa mengine 170 katika manispaa yote ya shinyanga.

Ameongeza kwenye ujenzi wa miundombinu, kuwa amejenga daraja la Nwangobeko kwenda Gharamba na kwamba ataendelea zaidi kuboresha miundombinu ya barabara ili wananchi wasipate tabu kufanya shughuli za kiuchumi.

Amegusia pia suala la umeme kwamba kijiji cha Gharamba akikuwa na umeme kabisa lakini sasa hivi huduma hiyo ipo, na kwamba katika vitongoji 84 vya manispaa ya Shinyanga kabla ya kuwa Mbunge viwili tu ndiyo vilikuwa na umeme,sasa hivi idadi kubwa umeme upo, huku vijiji 17 awali vitatu tu ndiyo vilikuwa na umeme sasa hivi vimesalia 4 tu ndiyo havina huduma hiyo.

“nawaombeni sana wananchi wa Kolandoto siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mpingieni kura nyingi za ndiyo Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan, nipigieni mimi niwe Mbunge wenu na Moses Mshangatila ili awe diwani wenu na tuwaletee maendeleo zaidi,”amesema Katambi.
Ameongeza kuwa, kwa upande wa sekta ya maji maeneo mengi yana maji, na yaliyosalia huduma hiyo itafika sababu wameshapata pesa sh.bilioni 196 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya maji ambayo itafika hadi Kata ya Kolandoto.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe, akizungumza kwenye mkutano huo wa kampeni, amewasisitiza wananchi kwamba siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 wajitokeze kwa wingi kupiga kura na kuwachagua wogombea wote wanatokana na CCM,kuanzia Madiwani,Mgombea Ubunge Patrobas Katambi na Rais,Dk.Samia Suluhu Hassan.

TAZAMA PICHA👇👇
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM Patrobas Katambi akinadi sera la ilani ya CCM kwa wananchi wa Kolandoto.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi (kulia)akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya Kolandoto Moses Mshagatila kwa wananchi.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akizungumza.



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464