Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi nakala ya fomu za uteuzi kwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT - WAZALENDO), Mhe. Luhaga Joelson Mpina.
Amekabidhiwa Fomu hizo leo Septemba 13,2025.
Mpina aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej
baada ya wagombea hao kuteuliwa na Tume kuwania nafasi hizo katika uchaguzi Mkuu wa utakao fanyika Oktoba 29, 2025.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464