
Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Viwandani wakiwa eneo lilipotokea tukio la mtoto mchanga kukutwa mwili wake umetupwa kwenye mfuko wa takataka

Mwenyekiti wa Mtaa wa Viwandani Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Ashraf Majaliwa akizungumzia tukio hilo.
Katika tukio la kusikitisha mwili wa mtoto mchanga ambaye anaekadiriwa kuwa na miezi nane umekutwa ndani ya mfuko wa takataka nje ya hosteli ya wanafunzi katika mtaa wa viwandani Manispaa ya Shinyanga na kusababisha taharuki kwa wananchi wa eneo hilo.
Tukio hilo limebainika wakati mmoja wa wananchi Jeremia Evansi alipokuwa anatafuta mabaki ya vyakula kwenye mifuko ya takataka kwa ajili ya kuku,alikuta mwili wa mtoto mchanga na kisha kuwajulisha watu wanaoishi kwenye nyumba ilipokutwa mifuko ya taka ambao mmoja ulikuwa na mwili wa mtoto mchanga.
"wakati na pitapita katika mifuko kutafuta chakula nikakuta mfuko ndani yake ulikuwa na taka na baada ya kufungua nikakuta kichanga ndani, mimi huwa ninatenda ya kulisha kuku soko la nguzo nane nilikuwa natafuta mabaki ya vyakula” amesema Evance.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Viwandani Ashraf Majaliwa amesema kitendo hicho ni ukatili mkubwa na kuwataka wanawake na mabinti kuepuka vitendo vya aina hiyo ambavyo vinakiuka haki za binadamu na nikinyume cha sheria.
Majaliwa amesema mtoto huyo mchanga alitolewa kwenye mfuko wa taka na kuwekwa kwenye boski na baada ya polisi kufika walichukuwa mwili huo.
Jeshi la polisi limefika eneo la tukio na kuchukua mwili huo kwa uchunguzi zaidi ili kubaini muhusika aliyefanya ukatili huo.

Jeremia Evansi mkazi wa Matanda ambaye alibaini uwepo wa mwili wa mtoto mchanga kwenye mfuko wa taka wakati akitafuta mabaki ya vyakula kwa ajili ya kuku.




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464