Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MGOMBEA Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo jipya la Itwangi Azza Hillal Hamad, leo Septemba 13,2025 anazindua Rasmi kampeni zake kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi wa Jimbo hilo, ili wamchague awe Mbunge wao, pamoja na kumpigia kura nyingi za ushindi Mgombea Urais, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Mkutano huo wa kampeni unafanyika katika eneo la Didia wilayani Shinyaga, na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi,wana CCM pamoja na Wagombea Udiwani.