SANTA EDWIN YAANZA KUPOKEA WATOTO WA BWENI
Mwandishi wetu
Mwanza
Shule ya awali na Msingi ya Santa Edwin (Pre and Primary) rasmi sasa kutoa huduma za kutwa na bweni ili kukuza taaluma Shuleni hapo.
Akiongea kwenye mahafali ya pili ya Shule hiyo Mgeni rasmi Julius Magembe, Afisa Taaluma Jiji la Mwanza amesema kuwa, Kwa sasa Shule hiyo ya Santa Edwin imeanza rasmi kutoa huduma za bweni Kwa wanafunzi Shuleni hapo.
" Nampongeza Kwa dhati Mkurugenzi wa Santa Edwin Bwana Edwin Soko pamoja na uongozi wote wa shule ukiongozwa na Mwalimu Mkuu Hassan Iibrahimu Kwa kazi nzuri mnayoifanya na kuiwezesha shule kuwa ya kutwa na Bweni" Alisema Magembe.
Magembe aliwapongeza pia walimu Kwa Shule hiyo Kwa matokeo mazuri wanayoyapata na kuwataka kuendelea kuitangaza shule Kwa kuwa na matokeo mazuri kama inavyofanya sasa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shule ya Santa Edwin Bwana Edwin Soko aliwahakikishia wazazi kuwa, shule itaendelea kusimamia malezi Bora Kwa watoto wote Shuleni hapo pamoja na matokeo mazuri kwenye mitihani yote.
Soko pia aliwaambia wazazi kuwa, shule itaendelea kutoa ufadhili Kwa watoto wasio na uwezo ili kusaidia kupata elimu Bora kupitia mpango Maalumu wa shule ya kusaidia familia zisizo na uwezo wa kusomesha watoto kwenye shule za mchepuo wa kiingereza.
"Ndugu Mgeni rasmi Kwa sasa Shule inasaidia watoto ishirini (20) kuwasomesha bure na tuna mpango wa kuongeza idadi hiyo ili jamii iweze kunufaika hasa watoto wa kike , tunafanya hivi ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu za kumuinua mtoto wa kike Kwa kuhakikisha anapata elimu kama mtoto wa kiume" alisema Soko.
Hii ni mahafali ya pili Kwa Shule ya Santa Edwin ya kwanza ilikuwa Mwaka jana 2024.
Shule ya Santa Edwin imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani mbalimbali kuanzia kata, Wilaya na Taifa.
Shule ya Santa Edwin ipo kata ya Majengo Mapya, Nyegezi, Kata ya Mkolani, Wilaya ya Nyamagana, Jijini Mwanza. shule inapokea watoto wanaohamia kwa madarasa yote yasiyo na mitihani.
Kwa mawasiliano
0754551306
0786349813
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464