` TAMASHA SIKU YA WANA HAPATOSHI SHINYANGA KUTUMIKA KUTAMBULISHA WACHEZAJI WAPYA WA TIMU YA STAND UNITED

TAMASHA SIKU YA WANA HAPATOSHI SHINYANGA KUTUMIKA KUTAMBULISHA WACHEZAJI WAPYA WA TIMU YA STAND UNITED


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

TAMASHA la Siku ya Wana linatarajiwa kufanyika Oktoba 4, mwaka huu, katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, ambapo pamoja na burudani mbalimbali,pia kutafanyika utambulisho wa wachezaji wapya wa Stand United kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi ya Championship.
Chrispin Kakwaya.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 25,2025 na Mwenyekiti wa Tamasha hilo Chrispin Kakwaya, wakati akitoa taarifa ya vyombo vya habari juu ya maandalizi ya Tamasha.

Amesema,tamasha hilo ni sehemu ya sherehe kwa wapenzi na mashabiki wa Timu ya Stand United,kuanzia muda wa Asubuhi hadi saa 12 jioni, ambapo kutakuwa na michezo ya Mbio za Baiskeli kwa wanaume na wanawake, nyimbo kutoka kwa wasanii mbalimbali Kanda ya Ziwa na wenyeji wa Shinyanga.

Amesema, pia kutakuwa na michezo ya utangulizi kati ya timu ya Bajaji na Bodaboda, Soko Kuu na Soko la Majengo pamoja na Dabi ya Upongoji FC na Ibinzamata.

Amesema baada ya hapo kutakuwa na utambulisho wa wachezaji wapya, ambao wamesajiliwa kuichezea Timu ya Stand United, na kutafuatiwa na mtanange kati ya Stand United na Timu moja ambayo inashiriki kucheza Ligi kuu ambayo wataitaja siku zijazo.

“Natoa wito kwa wananchi na wapenzi wote wa Timu ya Stand United,Mashirika na Taasisi mbalimbali, wajitokeze kwa wingi kwenye Tamasha hili la Siku ya wana ili kuingua Timu yao,ambalo litafanyika Uwanja wa CCM Kambarage na kutakuwa na kiingilio mzunguko sh.5,000,VIP Sh.10,000 na VVIP watakuwa na kadi maalum,”amesema Kakwaya.

Aidha,amesema tamasha hilo litatanguliwa pia na “Jonging”.
Ramadhan Zorro.

Kwa upande wake, Msemaji wa Stand United, Ramadhan Zorro, ametamba kuwa tamasha hilo litakuwa la aina yake tofauti na Matamasha mingine yaliyotanguliwa kutoka kwa Timu zingine, na kutoa wito kwa wananchi waje kwa wingi kuona kikosi ambacho wamekisajili.

Ametoa wito pia kwa Taasisi na Mashirika mbalimbali, kwamba wajitokeze kuidhamini Timu hiyo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464