` MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI PATROBAS KATAMBI AENDELEA NA KAMPENI ZA KUNADI SERA NA ILANI YA CCM KUOMBA KURA KWA WANANCHI

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI PATROBAS KATAMBI AENDELEA NA KAMPENI ZA KUNADI SERA NA ILANI YA CCM KUOMBA KURA KWA WANANCHI


Xxxx

Mgombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi, ameendelea na kampeni zake leo katika Kata ya Chibe, akieleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuahidi kushughulikia changamoto zilizobakia.

Katika mikutano yake, Katambi amebaimisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,amefanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi ndani ya jimbo hilo.

Amewaomba wananchi wampatie ridhaa tena ya kuwa Mbunge wao ili aendelee kuwaletea maendeleo pamoja na kumpigia kura nyingi za ushindi Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na Madiwani wote wa CCM,sababu Chama hicho ndicho chenye kuwaletea maendeleo wananchi.

Aidha,Mikutano ya Kampeni ya Katambi,imekuwa ikihudhuriwa na wananchi kwa wingi, hali ambayo inaashiria bado wanaimani naye katika kuwaletea maendeleo

Oktoba 29 ni Uchaguzi Mkuu, wa kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464