Shule ya Awali na Msingi Kom,imefanya mahafali ya tano kwa wanafunzi kuhitimu elimu msingi,huku wazazi ambao wanasomesha watoto wao shuleni hapo wakipongeza ubora wa taaluma.
Mahafali hayo yamefanyika leo septemba 20,2025 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Mkurugenzi wa Kampuni ya ujenzi Geo Special Classic Woks LTD Dastan Sospeter.
Sospeter akizungumza kwenye mahafali hayo,amepongeza utoaji wa taaluma kwa wanafunzi, na kwamba hata yeye watoto wake wamesoma katika shule za Kom na wamefanikiwa na wameajiriwa.
Amesema Kom ni Mahali salama kwa wanafunzi kutimiza ndoto zao, na kuwasihi wazazi wasisite kupeleka watoto wao shuleni hapo.
"kwa furaha niliyonayo katika shule ya Kom kutokana na kufanya vizuri kitaaluma natoa zawadi kwa wahitimu wote 67 nawapa Offa ya kuwasaidia wazazi wenu kupunguza gharama,mtoto akisajiliwa kujiunga shule ya sekondari Kom natoa shilingi 100,000 kwa kila mtoto," amesema Dastan.
Aidha,amesema pia atachangia ununuaji wa Gesi kwa miezi iliyosalia kabla ya kufunga shule, pamoja na kununua Kopyuta mbili,printer na Projector,kwa ajili ya kuongeza mbinu za ufundishaji kwa njia za TEHAMA.
Mkurugenzi wa Shule za Kom Jackton Koyi,amewashukuru wazazi kwa kuendelea kuwa amini, na kuwapeleka watoto wao kusoma shule hizo za Msingi na Sekondari,na kwamba wamekuwa wakifanya vizuri kitaaluma.
Ametoa Offa kwa wazazi ambao watachukua fomu za watoto kujiunga na Shule ya Sekondari Kom, kwamba fomu zote amelipia ni bure.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Awali na Msingi Kom Pius Sayi, amesema shule hiyo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 616, Walimu 26 na Wafanyakazi wasio walimu ni 21.
Ametaja wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi ni 67 wasichana 32 na wavulana 35, huku wanafunzi wa awali ambao wanajiunga na darasa la kwanza mwakani wapo 46 wasichana 20 na wavulana 26.
Aidha,ametaja mafanikio ya shule hiyo Kitaaluma,kuwa wanafunzi wamekiwa wakifanya vizuri mitihani yao ya kitaifa ya darasa la Nne na la Saba na wote wamekuwa wakifaulu.
Ametaja mikakati ya shule hiyo kuwa ni kuendelea kuboresha mazingira ya shule,pamoja na wanafunzi wa mitahani darasa la Nne na la Saba wawe wanakaa bweni tu kwa ajili ya kuwa andaa na mithani,huku wakijipanga pia kufundisha kwa njia ya TEHAMA..
Nao wahitimu akiwamo Kareny Peter, wamesema watafanya vizuri katika mitihani yao ya kitaifa ya kuhitimu elimu ya msingi na wote watafaulu kwa madaraja ya juu.
TAZAMA PICHA👇
Mkurugenzi wa Kampuni ya ujenzi Geo Special Classic Woks LTD Dastan Sospeter akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mkurugenzi wa Shule za Kom Jackton Koyi akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Awali na Msingi Kom Pius Sayi,Aakisoma taarifa ya shule.