` WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA JIMBO LA SHINYANGA MJINI WAJENGEWA UWEZO

WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA JIMBO LA SHINYANGA MJINI WAJENGEWA UWEZO

 





WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA WAJENGEWA UWEZO

NA EUNICE KANUMBA SHINYANGA

IKIWA ni maandalizi  kuelekea  uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi October mwaka 2025, jumla ya  wasimamizi wasaidizi  34  wa ngazi ya kata jimbo la Shinyanga  wamejengewa uwezo leo tarehe 4 August lengo likiwa ni kusimamia uchaguzi mkuu  unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 october 2025 kwa weledi.

Akizungumza wakati wa ufungunzi wa mafunzo hayo msimamizi wa uchaguzi jimbo la Shinyanga mjini Ally Lihuye amewataka watendaji hao kufuata sheria na taratibu na miongozo ya tume hiyo pasipo kuwajibuika kwa mamlaka nyingine kwani tangu walipoteuliwa kwa ajili ya utekelezaji wa jukumu hilo wamekuwa ni watumishi wa muda wa tume huru ya uchaguzi .

 “Tume iliwaridhia wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata    kutekeleza kazi za  uchaguzi Mkuu wa mwaka  2025 ambapo uteuzi wenu  umezingatia masharti ya kifungu cha sita(1),(2) na 5  na kifungu cha nane ( 1) na( 2) vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani”amesema  Lihuye

 Lihuye pia amewashihi watendaji hao kujiepusha    kuwa vyanzo vya malalamiko utoka kwa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi  pia wahakikishe wanazingatia ipasavyo katiba ,shera,kanuni ,miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na tumen a kuanisha kuwa    vyama vyote vya  siasa  vilivyo na usajili vishirikishwe  kwa ukamilifu kwa hatua zote kwa kuzingatia matakwa ya katika,sheria,kanuni na maelekezo.

Katika hatua nyingine  wasimamizi wasaidizi hao 34 katika ngazi ya kata   leo wamekula kiapo cha kujitoa kwa muda katika ushiriki wa chama chochote cha siasa  pamoja na kutunza siri zitokanazo na mchakato wa uchaguzi  kiapo kilichosimamiwa na  Agness Mlimbi ambaye ni hakimu  mkazi  wa mahakama  hakimu mfawidhi katika ngazi ya wilaya.









Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464