` MWENGE WA UHURU KUMULIKA MIRADI TISA YA BILIONI 1.6 MANISPAA YA SHINYANGA

MWENGE WA UHURU KUMULIKA MIRADI TISA YA BILIONI 1.6 MANISPAA YA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MWENGE wa Uhuru katika Manispaa ya Shinyanga utakimbizwa umbali wa kilomita 116.5 na kupita katika miradi 9 ya Maendeleo yenye thamani ya sh.bilioni 1.6.

Mwenge huo katika Manispaa ya Shinyanga, umepokelewa leo Agosti 7,205 ukitokea Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akizungumza mara baada ya kupokea Mwenge huo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Kalekwa Kasanga,amesema ukiwa katika Manispaa hiyo utazindua na kuweka mawe ya msingi miradi 9 ya sh.bilioni 1.6.

Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu inasema"Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu 2025 kwa Amani na utulivu.

Ambapo Mbio hizo za Mwenge Uhuru,zinakimbizwa na kiongozi wake Ismail Ali Ussi.

TAZAMA PICHA MIRADI AMBAYO IMEPITIWA NA MWENGE👇
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464