SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Ally Salum, ambaye pia ameshinda kura za maoni kutetea kiti chake, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai kilichotokea tarehe 06 Agosti 2025.
Kwa hakika taifa limepoteza kiongozi shupavu, mwenye hekima, busara, na mchango mkubwa katika kuimarisha misingi ya demokrasia na utawala bora. Mhe. Ndugai alikuwa kielelezo cha uzalendo, uvumilivu na uadilifu katika utumishi wa umma.
Mhe. Ahmed Ally Salum, anatoa pole kwa familia ya marehemu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), wananchi wa Kongwa, pamoja na Watanzania wote walioguswa na msiba huu mkubwa.
Aidha, anamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.
“Tutamkumbuka daima kwa uongozi wake uliotukuka na moyo wake wa kizalendo.”
Imetolewa Na.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la solwa
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464