Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter N.Masindi akizungumza kwenye ziara yake ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Mwataga,Kishapu na Kata ya Uchunga Agosti 25,2025
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, amesikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata za Mwataga, Kishapu na Uchunga katika mkutano wa hadhara uliofanyika Agosti 25, 2025 katika maeneo hayo.
Miongoni mwa changamoto zilizowasilishwa ni huduma ya maji safi, upatikanaji wa umeme, uboreshaji wa barabara,uboreshaji wa miundombinu ya mawasiliano ya simu Uchunga, huduma za afya katika Zahanati ya Lubaga na ujenzi wa nyumba ya walimu katika Shule ya Msingi Lubaga.
"Ndugu zangu wananchi niwapongeze kwa kuendelea kuiamni serikali ya awamu ya sita na pia napenda kuhamasisha kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kuepuka mikusanyiko isiyo na tija na kuwekeza zaidi katika familia zenu hususa ni katika maendeleo ya wanawake na watoto" amesema Masindi
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu, David Mashauri,akijibu maswali ya sekta ya elimu amesema Halmashauri imeanza kupokea fedha kwa ajili ya kujenga Shule shikizi katika maeneo yenye changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu huku Kitongoji cha Lubaga kilichoko Kata ya kishapu kikiwa ni miongoni wa wanufaika.
Kwa upande wa umeme, Mwakilishi wa Meneja wa TANESCO Wilayani humo, Gidion Kanan, amesema serikali inaendelea kusambaza nishati hiyo kwenye Vijiji na vitongoji kote Wilayani humo.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kulinda miundombinu ya umeme na kuunga mkono matumizi ya nishati safi ili kutunza mazingira.

Muonekano wa Awali wa choo kilichokuwa kikitumiwa na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lubaga iliyoko Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga

Muonekano wa choo cha kisasa kinachojengwa katika Shule ya Msingi Lubaga Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shimyanga kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga

"Ndugu zangu wananchi niwapongeze kwa kuendelea kuiamni serikali ya awamu ya sita na pia napenda kuhamasisha kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kuepuka mikusanyiko isiyo na tija na kuwekeza zaidi katika familia zenu hususa ni katika maendeleo ya wanawake na watoto" amesema Masindi
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wazazi kuwasomesha watoto wao na kuwaendeleza kwenye vipaji mbalimbali waliofeli masomo huku wakiwawekeza zaidi kwenye malezi bora yenye kufuata maadili ya KiTanzania huku akiahidi mahitaji mengine ambayo hayapata utatuzi serikali inaendeleza jitihada ya kuzitatua kwa haraka ili wananchi wanufaike na nchi yao.
Katibu Tawala Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Bi.Fatma Mohamed akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter N.Masindi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Mwataga,Kishapu na Kata ya Uchunga Agosti 25,2025

Mashauri ameongeza kuwa Shule ya Msingi Bukingwa-Mandenge na Bulima tayari zimepangiwa fedha kwa ujenzi wa madarasa, huku nyumba ya Walimu Shule ya Msingi Lubaga ikiwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 wanasubiria fedha ili kuboresha jengo hilo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kishapu Mkoani Shinyanga David Mashauri akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter N.Masindi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Mwataga,Kishapu na Kata ya Uchunga Agosti 25,2025

Meneja wa RUWASA Wilayani humo, Dickson Kamazima, amesema serikali inaendelea kusogeza huduma ya maji safi kwa wananchi ambapo kwa Kitongoji cha Mwataga utekelezaji umefikia asilimia 95, na maeneo mengine yatapatiwa huduma kupitia maji ya Ziwa Viktoria na visima vinavyochimbwa kisasa.
Aidha amesema wiki ya kwanza ya Septemba watafanya uthamini katika Kitongoji cha Migunga ili kusogeza huduma hiyo kupitia kwenye bomba kubwa la maji linaloelekea Kata ya Lagana, huku Kitongoji cha Mwanulu kikiwa kwenye mpango wa kusogezewa huduma pia baada ya kupokea fedha kutoka serikalini.
Meneja wa RUWASA Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Dickson Kamazima akijibu maswali ya wananchi kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter N.Masindi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Mwataga,Kishapu na Kata ya Uchunga Agosti 25,2025

Kwa upande wa umeme, Mwakilishi wa Meneja wa TANESCO Wilayani humo, Gidion Kanan, amesema serikali inaendelea kusambaza nishati hiyo kwenye Vijiji na vitongoji kote Wilayani humo.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kulinda miundombinu ya umeme na kuunga mkono matumizi ya nishati safi ili kutunza mazingira.
Wananchi wameendelea kuzipongeza jitihada za serikali kwa kusogeza huduma muhimu za kijamii jambo linalosaidia kujenga jamii bora na yenye matumaini imara.
Mwakilishi wa Meneja wa Tanesco Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Gidion Kanan akijibu maswali ya wananchi kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter N.Masindi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Mwataga,Kishapu na Kata ya Uchunga Agosti 25,2025
Afisa Tarafa ya Kishapu Mkoani Shinyanga Tano John ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter N.Masindi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Mwataga,Kishapu na Kata ya Uchunga Agosti 25,2025