Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MGOMBEA Ubunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Paschal Katambi,amerejesha Fomu za kugombea Ubunge, katika Tume Huru za Taifa za Uchaguzi kwa msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Shinyanga.
Amerejesha Fomu hizo leo Agosti 27,2025 huku akisindikizwa na Maelfu ya Wanachama wa CCM, kwa kuzunguka mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga na kukomea eneo la Karogo,na kisha kumuacha arejeshe Fomu hizo INEC akiwa na Viongozi wa CCM.
Katambi, akizungumza mara baada ya kurejesha Fomu hizo,amewashukuru Wana CCM kwa mapenzi makubwa walioonyesha kwake na kumuamini kuendelea kutetea kiti chake na kuahidi kwamba hatowaangush,bali atendelea pale alipoishia kuwaletea maendeleo wananchi na kukiheshimisha Chama.
"Mmenikopesha Imani,nitafanya kazi na nitakuwa mlinzi wa Katiba ya Nchi, Katiba ya Chama, kulinda Demokrasia na Mlinzi wa Haki na Utawala Bora na Shimyanga itaendelea kupiga hatua kubwa ya maendeleo," amesema Katambi.
"Nipo tayari kuwatumikia wananchi wa Shinyanga,nitumeni,uwezo ninao na nia niyo ya kuwaletea maendeleo,"Butababa" sitawaangusha na rudia tena sitawaangusha,"ameongeza Katambi.
Aidha,amesema wakati wa Kampeni ikifika wao kama CCM wataeleza ambacho wamekifanya ndani ya miaka mitano iliyopita,na nini wataendelea kufanya kwa wananchi.
"Leo tulichokifanya wakati wa kurejesha Fomu ni Mvua za rasharasha, bado Mvua zenyewe zinakuja na hiyo ni salama kwa wapinzani kwamba CCM tunakwenda kushinda kwa kishindo kwa nafasi za Udiwani,Ubunge na kura nyingi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan," amesema Katambi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe,amewataka Wana CCM kuendelea kuwa wamoja na mashikamano, pamoja na kuvunja makundi yaliyokuwapo kipindi cha kura za maoni ili waungane kukipigania Chama na kupata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025.
TAZAMA PICHA👇👇
Mgombea Ubunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi akizungumza mara baada ya kurejesha Fomu za Uteuzi kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464