MWENGE WA UHURU UMEWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI MRADI WA MAJI BUZINZA WILAYANI SHINYANGA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MWENGE wa Uhuru,umeweka jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji Kijiji cha Buzinza Kata ya Lyabukande wilayani Shinyanga.
Mradi huo utanufaisha wananchi wa vijiji vya Buzinza,Mwamakalanga, Mapingili,Lyamidati na Kimandaguli kwa awamu ya kwanza.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismali Ali Ussi akizungumza lelo Agost 6,2025 mara baada ya kumaliza kiweka jiwe la msingi mradi huo,amewapongeza RUWASA kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ya kusambaza majisafi na salama kwa wananchi wa vijijiji.
"Nawaomba wananchi mtunze miundombinu ya mradi huu wa maji,Mwenge wa uhuru umeukagua na kupitia nyaraka zote upo vizuri na nipo tayari kuweka jiwe la msingi,"amesema Ussi.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga Mhandisi Emmael Nkopi,awali akisoma taarifa za mradi huo,amesema utanufaisha wananchi 7,894 wa Vijiji hivyo.
Amesema, gharama ya ujenzi wa mradi huo ni sh.bilioni 1.4 na utaondoa adha ya wananchi ya ukosefu wa majisafi na salama.
TAZAMA PICHA👇👇
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi akiweka jiwe la msingi ujenzi mradi wa maji Buzinza.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Shinyanga Emmael Nkopi akisima taarifa ya mradi huo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464