` SPIKA MSTAAFU JOB NDUGAI AFARIKI DUNIA

SPIKA MSTAAFU JOB NDUGAI AFARIKI DUNIA

 



Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha Spika Mstaafu na aliyewahi kuwa Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Yustino Ndugai, kilichotokea leo tarehe 6 Agosti 2025 Jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), ambaye amesema:

"Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika Mstaafu wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kilichotokea leo Jijini Dodoma. Natoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Kongwa, Wenyeviti wa Mungano, na wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mhe. Spika.

Bunge limeeleza kuwa linaendelea kushirikiana na Kamati ya Mazishi pamoja na familia ya marehemu kuratibu mipango ya mazishi, huku taarifa zaidi zikiendelea kutolewa kadri maandalizi yanavyoendelea.






Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464