` KITUMBO AREJESHA FOMU ZA UTEUZI KUGOMBEA UDIWANI KATA YA SHINYANGA MJINI

KITUMBO AREJESHA FOMU ZA UTEUZI KUGOMBEA UDIWANI KATA YA SHINYANGA MJINI

KITUMBO AREJESHA FOMU ZA UTEUZI KUGOMBEA UDIWANI KATA YA SHINYANGA MJINI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

Salum Shabani Kitumbo amerudisha Fomu za uteuzi kugombea Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Amerudisha Fomu hizo leo Agosti 27,2025 kwa msimamizi msaidizi wa Uchaguzi (INEC) Kata ya Shinyanga Mjini Simon Mashishanga, huku akisindikwa na wanachama wa CCM.

Kitumbo akizungumza mara baada ya kurudisha Fomu hizo,amesema anakishukuru Chama chake kwa kumuamini na kupitisha jina lake kugombea nafasi hiyo ya Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini,na kuahidi ataitendea haki katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Aidha,ameomba makundi yote yaliyokuwapo wakati wa kura za maoni za kumtafuta mshindi mmoja wa kugombea nafasi hiyo ya udiwani,kwamba yavunjike na kuungana kuwa kitu kimoja na kutafuta kura za ushindi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29,2025 kwa nafasi za Udiwani,Ubunge na kura nyingi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464