RUWASA SHINYANGA MMEMUHESHIMISHA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI:KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU ISMAIL ALI USSI
Na Marco Maduhu,KAHAMA
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ali Ussi, amewapongeza Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga,kwa utekelezaji wa Miradi ya Maji.
Ametoa pongezi hizo leo Agosti 4,2025 Wakati akizindua mradi wa usambazaji maji katika vijiiji vya Chona,Ubagwe na Bukomela vilivyopo Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.
Amesema,anawapongeza RUWASA kwa kusambaza maji vijijini, na kuwaondolea adha wananchi ya kufuata maji umbali mrefu,na kwamba wamemuheshimisha Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi hiyo ya Maji.
"Rais Samia Suluhu Hassan alivyoingia Madarakani aliahidi kutekeleza miradi ya maji na kuyafikisha hadi maeneo ya vijijini na ametekeleza kwa vitendo na hili RUWASA nawapongeza mmemuheshikisha Rais," amesema Ussi.
Ameongeza" katika Mradi huu tumeukagua kwa kina na kupitia nyaraka zote, hakuna ubabaishaji uko vizuri,na Mwenge wa Uhuru umeridhia kuuzindua."
Pia,amempongeza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela,na Timu yake yote ngazi ya wilaya, kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ya kupeleka huduma ya maji kwa wananchi.
Naye Meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili,awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa Maji, amesema vijiji hivyo vitatu Chona,Ubagwe na Bukomela vilikuwa na shida kubwa ya maji.
Amesema utekelezaji wa Mradi huo ulianza Februari 14,2024,na umekamilika rasmi Julai 28,2025 na chanzo chake ni Maji ya visima virefu vitatu vilivyochibwa kwenye vijiji husika na gharama zake ni sh.bilioni 1.4.
"Mradi una nufaisha Kaya zipatazo 961 zenye Watu wapatao 5,763 kupata huduma ya Maji Safi na Salama na Tayari wateja 21 wameunganishiwa huduma ya Maji majumbani mwao." amesema Mhandisi Magili.
Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Bukomela, wamesema Mradi huo wa Maji,umewaondolea adha ya kufuata maji umbali mrefu pamoja na kutumia Maji Masafi.
Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi akikata Utepe kuzindua mradi wa maji.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi akiziundua Mradi wa Maji.
Awali Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili akisoma taarifa ya mradi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi (kulia)akimpongeza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464