` UTEMI WA BUSIYA WAPOKEA MASHINE 10 ZA KUSAGA NAFAKA KUSAIDIA WANANCHI

UTEMI WA BUSIYA WAPOKEA MASHINE 10 ZA KUSAGA NAFAKA KUSAIDIA WANANCHI

UTEMI WA BUSIYA WAPOKEA MASHINE 10 ZA KUSAGA NAFAKA KUSAIDIA WANANCHI

Mtemi wa Busiya Ntemi Makwaia III amepokea mashine 10 za kusaga nafaka kwaajili ya kuwasaidia wakazi wa eneo Hilo lililopo wilayani kishapu mkoani Shinyanga.

Makwaia wa III amepokea mahine hizo za kusaga mahindi na kukoboa mpunga kutoka kwa Shirika la kutoa misaada la Qatar nchini Tanzania ikiwa ni msaada kwaajili ya wananchi wa Busiya.

Hafla ya kupokea vifaa hivyo imefanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na na baadhi ya wanachama wa Busiya pamoja na waandishi wa habari.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo, Mratibu wa Miradi kutoka Shirika la Usaidizi la Qatar Bw.Mohammed Ibrahim amesema kuwa mchango huu utasaidia kata 10 za Busiya na kuongeza uzalishaji katika eneo Hilo na kukuza mapato zaidi ambayo yatakuza maisha yao.

Kwa upande wake Ntemi makwai III ameishukuru Qatar Charity kwa msaada wao wa mashine za kusaga ambapo wamezipata kwa wakati kati ufaao kwani ni karibu msimu wa mavuno.

Aidha Ntemi Makwaia III amewataka wapokeaji wa mashine hizo kuzitumia vyema ili kupitia mapato ambayo yatapatikana kutoka kwao, yaweze kufadhili sherehe za kila mwaka za Sanjo ya Busiya ambazo hufanyika kuanzia julai 1 na kilele ni julai 7.

Mashine hizo kumi (10) zitasambazwa kwenye kata 10 zilizopo kwenye utemi wa Busiya ambazo ni Ibadakuli, Kolandoto, Itilima, Talaga, Ukenyenge,Mwaweja, Kiloleli, Ngofila, Mwamashele na Lagana.

Tukio Hilo limefanyika ikiwa ni siku 20 zimepita toka Ntemi makwaia III 8Asimikwe Rasmi kuwa mtemi wa Busiya wa 24 akichukua nafasi ya Ntemi Edward makwaia II aliyestaafu
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464