` UTEMI WA BUSIYA WAPATA CHIFU MPYA

UTEMI WA BUSIYA WAPATA CHIFU MPYA

UTEMI WA BUSIYA WAPATA CHIFU MPYA

Utemi wa Busiya uliopo wilayani kishapu mkoani Shinyanga umempata mtemi mpya Ntemi Makwaia wa III Ambaye amesimikwa rasmi siku ya Jumamosi kwenye Ikulu ya Busiya iliyopo ukenyenge kuwa mtemi wa 24 wa Busiya na kuanza majukumu yake Rasmi.

Busiya imemsimika Ntemi makwaia wa III baada ya Mtemi aliyekuwepo Ntemi Edward makwaia kuomba kustaafu baada ya kuwa Mtemi kwa miaka 16 toka mwaka 2009 -2025.

katika hotuba yake ya kwanza Baada ya kusimikwa Ntemi Makwaia wa III alisisitiza neno moja kwa watu wa Busiyo wawe na UPENDO ili kuijenga Busiya imara zaidi .

Kwa upande wake Mstaafu Ntemi Edward makwaia aliahidi kuwa amepumzika kuwa Mtemi lakini bado yeye ni mwana Busiya na ataendelea kushirikiana na mtemi mpya na kushiriki shughuli zote za Busiya na kuwaomba viongozi wa utemi wa wanachi kumuunga mkono Ntemi Makwaia wa III ili aweze kufanya vizuri kuiendeleza Busiya .

Tukio la kumsimika limehudhuriwa na Balozi wa ufaransa nchini Tanzania watemi mbalimbali, viongozi wa serikali na Dini
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464