` WAGOMBEA 20,000 WAJITOKEZA CCM UCHUKUAJI FOMU

WAGOMBEA 20,000 WAJITOKEZA CCM UCHUKUAJI FOMU

 "Wagombea 20,000 wajitokeza CCM, uchukuaji fomu wavunja rekodi"

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema waliochukua fomu kuomba ridhaa ya ubunge kupitia majimbo Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar ni wanachama 4,109.

Kimesema kati yao waliochukua Bara ni wanachama 3,585 na Visiwani Zanzibar ni 524.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla, ameyasema hayo leo Julai 3, 2025 wakati akitoa taarifa ya mchakato wa CCM wa uchukuaji fomu uliofanyika kwa siku tano kuanzia Juni 28, 2025 na kuhitimishwa Julai 2, 2025.

“Chama Cha Mapinduzi kimefurahishwa na hamasa kubwa iliyojitokeza katika mchakato huu. Ninyi ni mashahidi uchukuaji wa fomu CCM safari hii umevunja rekodi, habari ya mjini ni uchukuaji fomu CCM.

SOMA ZAIDI CHANZO NIPASHE
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464