` SANTIEL KIRUMBA,CHRISTINA MNZAVA WAIBUKA KIDEDEA UBUNGE VITI MAALUM SHINYANGA

SANTIEL KIRUMBA,CHRISTINA MNZAVA WAIBUKA KIDEDEA UBUNGE VITI MAALUM SHINYANGA

PICHA NA MALUNDE BLOG

Santiel Kiruba,Christina Mnzava waibuka kidedea Ubunge Viti Maalum Shinyanga


SANTIEL Kirumba na Christina Mnzava, wameibuka washindi wa nafasi za Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi uliofanyika jana Julai 30, 2025.

Uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga, ukisimamiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Halima Dendego.

Katika uchaguzi huo ambao uliwahusisha wagombea wanane, Kirumba alipata kura 730, huku Mnzava akipata kura 719, na hivyo kuwashinda wagombea wengine kwa nafasi hizo mbili za ubunge wa Viti Maalum kupitia CCM.

Wagombea wengine waliowania nafasi hizo ni Salome Makamba amepata kura 216, Mwanahamishi Munkunda kura 196, Felister Buzuga kura 34, Alice Kyanila kura 29, Christina Gule kura 23 na Queneelizabeth Makune kura 19.

Jumla ya wajumbe 1,036 kutoka wilaya tatu za mkoa huo walishiriki uchaguzi huo, wakiwemo wajumbe 440 kutoka Wilaya ya Kahama, 227 kutoka Kishapu na 133 kutoka Manispaa ya Shinyanga.


PICHA NA MISALABA MEDIA





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464