
Huu ndio udhaifu wa mume wangu lakini nimepambana nao!
Jina langu ni Jesca kutokea Tanga, ninakoishi na familia yangu, nimeolewa na mwanaume mzuri anayefanya kazi na chombo cha habari huko Dar es Salaam, wakati mimi nafanya kazi katika Hoteli moja jijini hapa.

Kufanya kazi katika hoteli sio rahisi kwani kila siku narudi nyumbani nikiwa nimechoka sana na siwezi kumtunza mume wangu vizuri ingawa hajawahi kulalamika kuhusu hilo.
Hata hivyo, mwaka jana lilitokea jambo baya nyumbani kwetu likihusisha dada wa kazi na mume wangu, msichana huyu alichukua nafasi yangu kama mke, kuna kipindi hufua nguo zake za ndani na kuzianika bafuni ambapo mume wangu huoga pia.