` ACT-WAZALENDO:KUSUSIA UCHAGUZI NI KUWAPA USHINDI CCM WA KUPITA BILA YA KUPINGWA

ACT-WAZALENDO:KUSUSIA UCHAGUZI NI KUWAPA USHINDI CCM WA KUPITA BILA YA KUPINGWA

ACT-Wazalendo: kususia uchaguzi ni kuwapa ushindi CCM wa kupita bila kupingwa

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

CHAMA cha ACT-Wazalendo,kimesema kwamba,kususia Uchaguzi Mkuu 2025 ni kukipatia Chama Cha Mapinduzi (CCM)ushindi wa kupita bila ya kupingwa, na kusababisha kupata viongozi wabovu wasiojali maslahi ya wananchi.
Hayo yamebainishwa leo Julai 6,2025 na Kiongozi wa Chama hicho Dorothy Semu,wakati akizungumza na wananchi wa Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara.

Amesema, Chama hicho kimejipanga kushiriki uchaguzi Mkuu wa 2025 na kwamba watashinda nafasi zote za uwakilishi na hawawezi kususia uchaguzi huo,sababu CCM watapita bila ya kupingwa na kusababisha kuendelea kupata viongozi siyo matakwa ya wananchi.

"Kususa uchaguzi, ni kusababisha wagombea wa CCM kupita bila ya kupingwa,sisi ACT-Wazalendo tutashiriki uchaguzi kwa maono ya kutetea na kulinda Demokrasia ya nchi,"amesema Dorothy.
Amesema katika uchaguzi huo,watawaletea wananchi Wagombea wenye sifa ambao watajali maslahi yao.

Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Chama Cha ACT-Wazalendo Abdul Nondo,amekazia suala ya kususia uchaguzi na kudai kwamba wanaosusia uchaguzi Mkuu huenda wamepenyezewa kitu kidogo ili Chama Cha CCM kipite bila ya kupingwa.
Amesema kwamba vyama ambavyo vimekuwa vikisusia uchaguzi, huwapatia fursa Chama Tawala kushika dola pamoja na kupitisha sheria ambazo zitawakandamiza wapinzani siku zote, kama iliyotokea kwa CUF huko Pemba.

Aidha,amewataka wananchi wa Shinyanga kwamba wasikubali propaganda za kususia uchaguzi, bali washiriki uchaguzi huo ili wapate viongozi wenye kujali maslahi hiyo,sababu watakaoumia siyo viongozi bali ni wao wenyewe.
Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Bara Isihaka Mchinjita,amewataka wananchi wa Shinyanga, kwamba wasifanye makosa kwenye uchaguzi mkuu,bali wachague viongozi ambao watabadili mustakabali wa maisha yao na kunufaika na Rasilimali za Madini.

Naye Naibu Waziri Kivuli Habari,Mawasiliano na TEHAMA ACT-Wazalendo Emmanuel Ntobi, wao hawakubaliani nchi kurudishwa kwenye mfumo wa Chama kimoja,kwa kususia uchaguzi, na ndiyo maana wameamua kushiriki uchaguzi huo ili kuendeleza mapambo ndani ya vita,na kuleta mapinduzi.

Kaimu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Shinyanga Hassan Ibrahimu,amewataka wananchi kwamba siku hiyo ya uchaguzi Mwezi Oktoba kuwa wakimaliza kupiga kura wazilinde.

TAZAMA PICHA👇👇
Kiongozi wa Chama Chama Cha ACT-Wazalendo Dorothy Semu akizungumza.
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Bara Isihaka Mchinjita akizungumza.
Naibu Waziri Kivuli, Habari,Mawasiliano na TEHAMA, ACT-Wazalendo Emmanuel Ntobi akizungumza.
Mwenyekiti wa Ngome ya vijana Chama Cha ACT-Wazalendo Abdul Nondo akizungumza.
Mkutano ukiendelea.
Awali Kiongozi wa ACT-Wazalendo Doroth Semu akiwasili kwenye Mkutano wa Hadhara kuzungumza na wananchi wa Shinyanga.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464