` KATAMBI ATEKELEZA AHADI AKABIDHI MILIONI 5 KWA TIMU YA STAND UNITED,AAHIDI MILIONI 10 WAKIPATA USHINDI KESHO DHIDI YA FOUNTAIN GATE

KATAMBI ATEKELEZA AHADI AKABIDHI MILIONI 5 KWA TIMU YA STAND UNITED,AAHIDI MILIONI 10 WAKIPATA USHINDI KESHO DHIDI YA FOUNTAIN GATE

KATAMBI ATEKELEZA AHADI AKABIDHI MILIONI 5 KWA TIMU YA STAND UNITED,AAHIDI MILIONI 10 WAKIPATA USHINDI KESHO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana,ametekeleza ahadi yake ya kukabidhi sh.milioni 5 kwa Timu ya Stand United,huku akiahidi kutoa tena sh.milioni 10 endapo wakipata ushindi dhidi ya Fountain Gate hapo kesho.

Amekabidhi fedha hizo leo Julai 7,2027, kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,ambaye pia ni mlezi wa Timu hiyo ya Stand United.
Amesema Julai 3 Mkuu wa wilaya alifanya kikao na wadau wa Timu ya Stand United, kwa ajili ya kutoa hamasa kwa wachezaji ili wapate ushindi katika mchezo wa Playoff wa nyumbani dhidi ya Fountain Gate,ambapo yeye aliahidi kutoa sh.milioni 5.

Amesema licha ya Stand United kupoteza mchezo huo wa nyumbani,kwamba ahadi yake ilikuwa ipo pale pale, kwa lengo la kuendelea kutoa hamasa kwa wachezaji ili wapate ushindi,na kwamba katika mchezo wa kesho wakipata ushindi ameahidi kutoa tena sh.milioni 10.
“Niliumia sana tulivyopoteza mchezo wetu wa nyumbani dhidi ya Fountain Gate,lakini hatukati tamaa,kesho timu yetu inakwenda kupata ushindi wa kishindo ugenini, na tutashiriki kucheza msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara,”amesema Katambi.

Amewaomba pia Mashabiki wote wa Timu hiyo, na kila Mwana Shinyanga, kwamba kila mmoja kwa dua yake waiombee timu yao, ili kesho ipate ushindi katika mchezo wao wa pili wa Playoff.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,amempongeza Katambi,na wadau wengine wa michezo ambao wamekuwa wakiguswa na timu hiyo, na hata kutoa pesa za hamasa, na kwamba hadi sasa wana Jumla ya sh.milioni 25.
Amesema Timu hiyo ina kikosi kizuri, na kupoteza mchezo wa kwanza ilikuwa ni ajali kazini, bali huko ugenini wanakwenda kufanya maajabu, na amesha zungumza na wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo.

Aidha,amesema kwa mashabiki ambao wapo tayari kwenda huko Manyara kwa ajili ya mechi hiyo,Magari yapo na kwamba ameshapewa maelekezo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita,kuwa mashabiki watakao kwenda huko watunzwe na kurudi salama.

Mchezo wa kwanza wa Playoff dhidi ya Stand United na Fountain Gate, ambao ulichezwa Mjini Shinyanga,Fountain Gate walipata ushindi wa Goli 3-1.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi (kushoto)ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu,akimkabidhi sh.milioni 5 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro kwa ajili ya kutoa hamasa kwa Timu ya Stand United.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464