` GUMZO SHINYANGA KATAMBI AKIRUDISHA FOMU KUTETEA KITI CHAKE CHA UBUNGE

GUMZO SHINYANGA KATAMBI AKIRUDISHA FOMU KUTETEA KITI CHAKE CHA UBUNGE

GUMZO SHINYANGA KATAMBI AKIRUDISHA FOMU KUTETEA KITI CHAKE CHA UBUNGE

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu,amerejesha Fomu ya kuomba ridhaa tena ya kuteuliwa na Chama chake cha CCM,Kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini katika Uchaguzi Mkuu 2025.

Amerejesha Fomu hiyo leo Julai 2,2025 katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Katambi akizungumza mara baada ya kurejesha Fomu hiyo,amesema bado ana nguvu ya kuwatumikia wananchi wa Shinyanga,Serikali,pamoja na Chama,na kwamba akipata ridha hiyo tena ya kuwa Mbunge,ataendelea kuwaletea maendeleo.

“Shukrani kwa Chama changu cha CCM,wananchi wa Shinyanga kwa kuniamini na kunipatia ridhaa ya kuwa Mbunge ndani ya miaka mitano iliyopita, na hapa Shinyanga nimefanya mambo makubwa ya kimaendeleo,”amesema Katambi.
Amemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini katika Utumishi wa Serikali na kumpatia nafasi ya Unaibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu, na yupo tayari kuendelea kuhuduma katika nafasi hiyo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464