TEMBO FC MABINGWA LIGI YA DUMISHA AMANI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
LIGI ya Dumisha Amani imetamatika katika viwanja vya shule ya Msingi Mwakanga wilayani Shinyanga,ambapo Timu ya Tembo FC wameibuka washindi wa Ligi hiyo.
Fainali hiyo imechezwa leo Julai 13,2025, kwa Timu mbili zilizoingia Fainali ambazo ni Tembo FC na Young Star,ambapo Timu 32 zilishiriki Ligi hiyo,kutoka Kata 14 za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mchezo huo hadi unatamatika dakika 90 Tembo FC waliibuka na ushindi wa Goli 2-0 dhidi ya Young Star, ambao hawakupata kitu,na hivyo kufanya Tembo Fc kuibuka mabingwa wa Ligi hiyo,ambapo Mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Fadison.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu wilaya ya Shinyanga Joseph Assey, amempongeza Mafadhili wa Ligi hiyo,kwamba ameibua na kukuza vipaji vya vijana,na kumuomba aendelee kufadhili michezo ili vijana waonyeshe vipaji vyao na hata kusajiliwa kwenye Timu kubwa.
Mgeni Rasmi katika ufungaji wa Ligi hiyo Kocha wa Timu ya Tanzania Prisons Amani Josiah,ameseme amefurahishwa na mashindano hayo na kuahidi kwamba atawasiliana na waratibu ili kubaini vijana ambao wamefanya vizuri kwa kuonyesha vipaji vyao ili aone namna ya kuwasaidia na hata kucheza Ligi kuu.
Pia,ametoa hadi kwamba kwa mashindano yajayo atatoa sh.milioni 5 ili kudhamini Ligi hiyo na kuendelea kukuza na kuibua vipaji vya vijana.
Nao baadhi ya Vijana walioshiriki Ligi hiyo,akiwamo Frank Ikobela,wamesema wameonyesha vipaji vyao, na kuomba wadau wa michezo waendelee kujitolea kufadhili michezo ili kuibua vipaji vyao sababu mpira ni Ajira.
Aidha,katika mashindano hayo Mshindi wa Kwanza ameibuka na Kitita cha sh.milioni 5,Jezi na Mipira,Mshindi wa Pili ametapa sh.milioni 3 Jezi na Mipira,Mshindi wa tatu amepata milioni 1.5 Jezi na Mipira, na Mshindi wa Nne amepata Laki 7.5 Jezi na Mipira.
Ligi hiyo ilianza kutimua vumbi kuanzia Juni 8 na imetamatika leo Julai 13,2025.
TAZAMA PICHA👇👇
Kocha wa Timu ya Tanzania Prisons Amani Josiah akizungumza.
Mwenyekiti wa SHIDIFA wilaya ya Shinyanga Joseph Assey akizungumza.
Kocha wa Timu ya Tanzania Prisons Amani Josiah akikabidhi Kombe kwa kiongozi wa Timu ya Tembo FC Frank Ikobela.
Kocha wa Timu ya Tanzania Prisons Amani Josiah akikabidhi Sh.milioni 5 kwa kiongozi wa Timu ya Tembo FC Frank Ikobela.