
Kwa majina naitwa Salma Naumu, natokea Tanga, ni mwanamke wa miaka 25, ni single mama wa mtoto mmoja, nilikaa mwaka mmoja baada ya kuachana na mzazi mwenzangu ndio nikaanzisha mahusiano na kaka mmoja.

Kaka huyo ni mtu wa Zanzibar, kwenye mahusiano yetu alikuwa ananijali sana mimi pamoja na mtoto wangu, kwa hilo simsemi vibaya ila shida aliyokuwa nayo ni mtu anayesusa sana.