` EMEDO YANADI MAFANIKIO YAKE KWENYE JUKWAA LA MASHARIKIANO

EMEDO YANADI MAFANIKIO YAKE KWENYE JUKWAA LA MASHARIKIANO


EMEDO YANADI MAFANIKIO YAKE KWENYE JUKWAA LA MASHARIKIANO

Mwandishi wetu,TANGA

Shirika la Environmental Management and Economic Development Organization (EMEDO)limeshiriki kikamilifu kikao Cha mashirikiano baina ya Asasi zisizo za Kiraia na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kwa kueleza mafanikio ya utekelezaji wa shughuli zake.katika Ziwa Victoria.
Afisa Mawasiliano wa EMEDO Peter Kimisha akishiriki hatua ya awali ya kueleza mategemeo ya Shirika kwenye mkutano huo aliweka bayana kuwa EMEDO inakiona kikao hicho kuwa ni fursa ya kueleza mbele ya wadau wengine utekelezaji wa kazi zake Kwa Mwaka 2025 - 2026 pamoja na kutengeneza mahusiano mkakati na wadau wengine.

Peter Pia alieleza umuhimu wa kikao hicho ni kuuelewa vyema muongozo wa mashirikiano baina ya Sekta ya Uvuvi na Asasi za Kiraia zinazofanya kazi kwenye eneo la uvuvi.
Naye Bwana Edwin Soko, Mjumbe wa Bodi wa EMEDO alitoa wasilisho zuri lililoeleza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Shirika la EMEDO kwenye eneo la uchumi na mazingira ndani ya sekta ya uvuvi.

Soko alitaja baadhi ya mafanikio ni kutekeleza vyema mradi wa kuzuia watu kuzama maji ndani ya Ziwa Victoria Kwa kueleza mafanio ya kutoa elimu kwa wavuvi, kugawa zana za uokozi ikiwemo kugawa makoti okozi Kwa wavuvi, kujenga vituo vya utabiri wa hali ya hewa Kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), kutoa mafunzo ya usalama kwa wavuvi na pia jamii kwenye maeneo ya upwa wa Ziwa Victoria na mashuleni

Soko pia alieleza mafanikio ya EMEDO katika upande wa uwezeshwaji wa mwanamke, ambapo alizungumza jinsi EMEDO imesaidia katika uanzilishi wa Mtandao wa Wanawake Wachakataji Tanzania (TAWFA), uundaji wa vikundi VICOBA na ujenzi wa chanja za kisasa wilayani Muleba Kwa ajili ya kukaushia dagaa ili kuongeza thamani ya mazao ya samaki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uvuvi Prof.Mohammed Sheikh aliishukuru EMEDO na mashirika mengine kwa kuitikia wito wa kikao hicho na kuweka bayana kuwa Wizara itaemdelea kufanya kazi bega Kwa bega na mashirika hayo.

Naye Mratibu wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Bwana Tumaini Chambua aliwasiliaha muongozo wa mashirikiano Kati ya Wizara na mashirika yasiyo ya kiserikali na kuwaomba washiriki kikamilifu kwenye kutoa mapendekezo ya ndani ya wiki mbili.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464