` BONDA NKINGA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KISHAPU

BONDA NKINGA AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KISHAPU

 

Na Marco Maduhu,KISHAPU

MJUMBE wa Mkutano Mkuu CCM Mkoa wa Shinyanga kupitia Kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu Bonda William Nkinga,amechukua Fomu na kuirudisha,ya kuomba ridhaa ya Chama chake,kumteuwa kugombea Ubunge Jimbo la Kishapu katika Uchaguzi Mkuu 2025.

Amechukua na kuirudisha Fomu hiyo leo Julai 1,2025, katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Kishapu, chini ya Katibu wa CCM wilaya hiyo Peter Mashenji.

Amesema, endapo akipata ridhaa ya Chama Chake kuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu,atawatumikia wananchi na kuwaletea mabadiliko chanya ya kimaendeleo,na kwamba anauzoefu  ndani ya Chama na Serikali.

TAZAMA PICHA👇👇

Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Mkoa wa Shinyanga kupitia Kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu Bonda William Nkinga (kulia)akikabidhiwa Fomu ya Ubunge na Katibu wa CCM wilaya ya Kishapu Peter Mashenji.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464