

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abdul Aziz Said Sakala, amepata baraka za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi ya Udiwani wa Kata ya Mjini, jimbo la Shinyanga Mjini.
Uamuzi huo umetolewa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM baada ya kupitia na kujadili majina ya wanachama waliowasilisha maombi ya kushiriki mchakato wa kura za maoni ndani ya chama.
Sakala sasa anaingia katika kinyang'anyiro cha kura za maoni akikabiliana na makada wengine wa CCM akiwemo Rahma Kwareri na Salum Kitumbo, ambapo mshindi atapeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu ujao.