Aliyekuwa Mhasibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Justine Kivambe, ameibuka kuwa mmoja wa wagombea waliojitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Jimbo la Kawe katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Justine Kivambe alianza safari yake ya kielimu katika Shule ya Sekondari Mzizima, mojawapo ya shule kongwe jijini Dar es Salaam. Baadaye alijiunga na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambako alipata elimu ya uhasibu na masuala ya fedha na kutokana na ufaulu wake, alipata nafasi ya kwenda kusoma nchini Japan, ambako alihitimu shahada ya juu katika masuala ya Usimamizi wa Fedha na Sera za Umma (Public Finance & Policy).
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464