BIDHAA MPYA YA JAMBO MWAMBA YAZINDULIWA RASMI
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Uzinduzi huo umefanyika leo, Juni 7, 2025, katika Viwanja vya Zimamoto vilivyopo jirani na Soko la Nguzonane, ndani ya Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kiongozi Mkuu wa Jambo Media, ambaye pia ni Kiongozi wa Ubunifu na Msimamizi wa Chapa wa Jambo Group, Nickson George, amesema kuwa bidhaa hiyo ni ya kipekee na imelenga kuwawezesha vijana kupata hamasa, kujiamini,na kuonyesha vipaji vyao kwa ujasiri.
“Kampuni ya Jambo Group tumekuwa tukifanya matamasha mbalimbali pamoja na kampeni maalum kwa ajili ya kuibua na kukuza vipaji vya vijana, kupitia uzinduzi wa bidhaa zetu, leo tumezindua kinywaji kipya cha Jambo Mwamba,”amesema George.
Ametoa wito kwa vijana kuendelea kushiriki katika matamasha ya Jambo ili kuendeleza na kutangaza vipaji vyao, huku akisisitiza kuwa hatua hiyo inaweza kusaidia kufanikisha ndoto zao.
Kwa upande wao baadhi ya vijana walioshiriki kwenye tamasha hilo la uzinduzi, wameishukuru Jambo Group kwa kuendelea kufanya majukwaa ya kuonyesha vipaji, wakieleza kuwa hiyo ni nafasi ya kipekee ambayo imekuwa chachu ya maendeleo yao.
Katika tamasha hilo, vipaji mbalimbali vilionyeshwa ikiwa ni pamoja na kuimba, kucheza, kupiga danadana, pamoja na kushiriki mashindano ya kula ugali,mikate, na kuvuta kamba.
Uzinduzi huo ulipambwa na burudani ya msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya Dvoice.
TAZAMA PICHA👇👇
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media,ambaye pia ni Kiongozi wa Ubunifu na Msimamizi wa Chapa wa Jambo Group, Nickson George,akizungumza.
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media,ambaye pia ni Kiongozi wa Ubunifu na Msimamizi wa Chapa wa Jambo Group, Nickson George akinada bidhaa mpya ya Jambo Mwamba.
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media,ambaye pia ni Kiongozi wa Ubunifu na Msimamizi wa Chapa wa Jambo Group, Nickson George akinada kinywaji kipya cha Jambo Mwamba.
Msanii wa kizazi kipya DVOICE akinadi kinywaji kipya cha Jambo Mwamba.
DVOICE akipiga Push-Up
Nickson George akipiga Push-Up.
Michezo mbalimbali ikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464