` DVOICE ANOGESHA UZINDUZI WA KINYWAJI KIPYA CHA JAMBO MWAMBA

DVOICE ANOGESHA UZINDUZI WA KINYWAJI KIPYA CHA JAMBO MWAMBA


DVOICE ANOGESHA UZINDUZI WA KINYWAJI KIPYA CHA CHA JAMBO MWAMBA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya,DVOICE, ameshiriki katika uzinduzi wa kinywaji kipya kinachojulikana kama Jambo Mwamba.
Uzinduzi huo unafanyika leo Juni 7,2025 katika Viwanja vya Zimamoto Nguzo nane Manispaa ya Shinyanga, ambao uliambatana pia na upigaji wa Push-Up 20, Kati ya DVOICE na Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George ambaye pia ni Kiongozi wa Ubunifu na Msimamizi wa Chapa Jambo Group.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wakazi mbalimbali wa Shinyanga, wakiwemo mashabiki wa muziki na wadau wa burudani, waliokuja kushuhudia uzinduzi huo wa aina yake.
Kinywaji hicho kipya cha Jambo Mwamba kinatajwa kuwa na ladha ya kipekee na kinalenga kuvutia watumiaji wa rika mbalimbali, huku kikisindikizwa na kampeni za ubunifu zinazolenga kushirikisha vijana na wasanii maarufu kama njia ya kukuza chapa hiyo sokoni.

Shughuli za uzinduzi bado zinaendelea katika viwanja hivyo, huku wakazi wakipewa fursa ya kuonja bidhaa hiyo mpya sambamba na kushiriki katika michezo, burudani na promosheni mbalimbali.
Endelea kufuatilia mtandao huu kwa taarifa zaidi na matukio ya picha kutoka katika uzinduzi wa Jambo Mwamba.

TAZAMA PICHA👇👇
Msanii DVOICE akinadi Kinywaji Kipya cha Jambo Mwamba.
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George ambaye pia ni Kiongozi wa Ubunifu na Msimamizi wa Chapa Jambo Group akinadi Kinywaji kipya cha Jambo Mwamba.
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George ambaye pia ni Kiongozi wa Ubunifu na Msimamizi wa Chapa Jambo Group akinadi Kinywaji kipya cha Jambo Mwamba.
DVOICE akipiga "Push-Up" 20.
DVOICE akipiga "Push-Up" 20.
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George ambaye pia ni Kiongozi wa Ubunifu na Msimamizi wa Chapa Jambo Group akipiga "Push-Up".
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media Nickson George ambaye pia ni Kiongozi wa Ubunifu na Msimamizi wa Chapa Jambo Group akipiga "Push-Up".

Endelea kufuatilia mtandao huu kwa taarifa zaidi na matukio ya picha kutoka katika uzinduzi wa Jambo Mwamba........

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464