


Na Kareny Masasy
WADAU Mkoani Shinyanga wameeleza teknolojia ya habari iliyoingia duniani
inatakiwa wazazi wawe makini katika suala la malezi na makuzi ya watoto
wao hasa matumizi ya mitandao ya kijamii
na luninga kwa kuangalia vipindi ambavyo
vitaweza kuwajenga kimadili.
Hayo yamesemwa leo Mei,2025 kwenye mjadala
uliokuwa unahusu Nafasi ya wazazi na walezi katika matunzo ya watoto” ambapo Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lyidia Kwesigabo
amesema kila mwaka mwezi Mei, Tanzania ina adhimisha siku ya familia
duniani ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu inasema Mtoto ni Malezi ;Msingi wa familia bora Taifa imara.
Mgeni rasmi katika mjadala huo Kaimu
katibu tawala mkoa wa Shinyanga David Lyamogi
amesema familia zilizopitia malezi bora
hazina changamoto kubwa katika malezi yao pindi wakiwa wakubwa hivyo jamii
inatakiwa ifahamu Malezi ya watoto ni muhimu yanaanzia pindi mama akiwa
mjamzito.
Kwesigabo amesema majadiliano yote
yaliyotolewa na wadau yatafanyiwa kazi
huku maadhimio yaliyotolewa kukutana mara kwa mara ili kuweza kujengana
kimawazo na kuimarisha hali ya malezi ya watoto kwenye familia katika mkoa huu.
Afisa Miradi kutoka Shirika la Invest in Children Society (ICS), Lucy Maganga
amesema kuna aina tofauti tofauti ya
familia ambapo kuna familia ya mama na
watoto,baba na mama na watoto, wanafamilia wanaoishi na watoto na majirani wote wanajumuishwa katika malezi
na kutoka mchango ulio chanya kwa watoto.
Maganga amesema watu kwa pamoja wanaweza kumfundisha mtoto mila na desturi nzuri ,maadili mema na stadi
mbalimbali ili mtoto aweze kukua bila kuwatenga kwa kuangalia jinsia zao.
Maganga anasema hakuna familia isiyokuwa na changamoto
hivyo lazima kuwepo na mawasiliano chanya kwa kila mmoja ili watu wote wajione
kuwa ni sehemu ya familia ili waweze kumpa malezi bora mtoto.
Mwandishi wa habari Anikazi Kumbemba akiwakilisha Mada kwa niaba ya klabu ya
waandishi wa habari (SPC) amesema
waandishi wa habari ni chachu ya
kuleta elimu kwenye jamii juu ya
teknolojia inayoingia duniani kwani
mataifa ya nje tayari yamekuwa yakitumia teknolojia habari kwa watoto wao.
Mwenyekiti wa watu wenye ulemavu wa
ngozi mkoani Shinyanga na Mjumbe wa
Shirikisho la watu wenye ulemavu
(Shivyawata) Unice Manumbu amesema
wapo wanawake wanaopewa ujauzito
na kukimbiwa wanapojifungua na wanalazimika
kwenda mitaani kuomba sababu ya
kukosa matunzo na kuwafanya watoto ndiyo
chanzo cha mapato.
Mwenyekiti wa Umoja wa vituo vya kulelea watoto mchana Damari Mollel
amesema wao wamekuwa ndiyo walezi
wakubwa watoto wazazi wako bize na shughuli zao wakumbuke wanapo muachia msichana wa kazi
mtoto ndiyo anakuwa na mawazo
aliyofundishwa msichana huyo awe na tabia nzuri au mbaya.
Mwenyekiti wa baraza la watoto Taifa Rafael Charles amesema mtoto akilelewa vizuri katika malezi
yanayotakiwa hata kushiriki kwenye masuala mbalimbali ya kijamii atakapo kuwa mkubwa ataweza kutoa mchango wake kulijenga taifa.
“Naishukuru serikali katika utoaji wa maoni katika dira ya maendeleo ya taifa
walishirikisha kundi la watoto na Programu Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya Awali
ya Mtoto
yamefikia katika ngazi ya Halmashauri na kata kwa
kuhakikisha mtoto anapata malezi yaliyobora na sahihi”amesema Charles.
Mwenyekiti wa baraza la wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano
amesema suala la watoto kwenye malezi
kuanzia umri wa mwaka sifuri hadi minane
wanaotakiwa kupata malezi bora hivyo
wazee nao wamekaa na kutathimini mmomonyoko wa maadili na kupinga ukatili wa
wanawake na watoto hasa mambo ya lishe.




.jpeg)







.jpeg)

MWISHO.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464