` UWT WILAYA SHINYANGA MJINI WASISITIZA MAADILI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

UWT WILAYA SHINYANGA MJINI WASISITIZA MAADILI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

 

Rehema Nhamanilo, Mwenyekiti UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Wanachama wa CCM wilaya ya Shinyanga wakifatilia Mkutano 

Diwani wa kata ya Ndala,Zamda shabani akiongea na wanachama wa CCM

Na Mwandishi wetu –SHINYANGA

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Rehema Nhamanilo ameonya wanachama wa jumuiya hiyo kuepuka kupokea zawadi za watia nia wa nafasi za ubunge na udiwani kwa lengo la kuwachagua kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu , kwani amesema kwa kufanya hivyo ni kuhalalisha rushwa

Nhamanilo ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM na jumuiya zakekatika kata za Mwamalili,Old Shinyanga,kizumbi,Ibinzamata na Ibadakuli ikiwa ni mwendelezo wa ziaraya kamati ya utekelezaji ya U.W.T Wilaya ya Shinyanga Mjini,ambayo imelenga kukagua uhai wa Chama.

Amesisitiza viongozi na wanachama kuepuka kupokea zawadi za watia nia wa nafasi za uongozi kwenyeuchaguzi Mkuu baadaye Mwaka huu,na badala yake wanapaswa kuwa mfano na kielelezo cha uadilifukwa kuzingatia miiko ya chama hicho,na kuongeza kuwa kwa kushiriki vitendo hivyo inachangiakurudisha nyuma maendeleo.

Amekemea pia kuhusu tabia ya kuchafuana na kudhoofishana kisiasa hasa katika kipindi hiki chakuelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais,wabunge na madiwani,na badala yake waendelee kushirikianana kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao,kwani ndiyo silaha ya ushindi.

Ametahadharisha kuepuka kampeini kabla ya wakati kwani kwa kufanya hivyo ni fujo na ukiukaji wamaadili ya chama lakini pia ni kuwakatisha tamaa na kuwadhoofisha kisaikolojia wabunge na madiwani waliopo madarakani,ambapo ametaka waachwe wakamilishe kipindi chao kilichobaki, na amesisitiza kuhusu misingi ya utu,heshima na ubinaadamu,”waacheni wafanye kazi,wakamilishe kipindi chao kilichobaki,msiwabeze viongozi waliopo madarakani,wasipuuzwe, subirini wakati wa kampeni utakapofika kuliko kuanza sasa”

Mwenyekiti huyo wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini amesema wakati utakapofika wanachama hao hasa wanawake wachukue fomu za kugombea ubunge na udiwani,kwani hiyo ndiyo demokrasia.

Kwa upande wake katibu wa UWT –CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Bi Getrude Mboyi amewakumbushaviongozi wa kata na matawi kuwajibikia jukumu la kusimamia uhai wa chama na wanachama kuhakikishawanalipa ada ili kuendelea kuimarisha uimara wa CCM na jumuiya zakeKatika ziara hiyo wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya UWT wilaya ya Shinyanga Mjini wamewasilishamada za maadili na uchaguzi,ukatili wa kijinsia,mahusiano na ushirikiano na jamii.

Ziara hiyo iliyoanza tangu Mei 12,2025 inatarajiwa kuhitimishwa Mei 19,2025 ambapo viongozi hao wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini watatembelea katika kata zote, na tayari viongozi haowamekwishatembelea kata za Ibadakuli,Kizumbi,Ibinzamata,Mwamalili na Old Shinyanga ambapo leoMei 15,2025 walikuwa chibe na Lubaga.








Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464