
Na Daktari Jane Kim, MD
Neva ya Vagus ni neva ndefu zaidi kati ya neva za fuvu la kichwa. Inatoka kwenye ubongo (brainstem) hadi kwenye kifua na tumbo. Inadhibiti kazi muhimu kama vile:Mapigo ya moyo ,Shinikizo la damu ,Kupumua ,Usagaji wa chakula 🍲
Iwapo neva hii itachochewa sana, inaweza kusababisha kushuka ghafla kwa mapigo ya moyo na shinikizo la damu, pamoja na dalili kama:Kizunguzungu ,Kichefuchefu ,Kutokwa jasho na Kuzimia kabisa (vasovagal syncope) 😵
🧬 UFANYAJI KAZI WA VASOGAL
Mwitikio wa vasovagal si wa ajabu, na njia zake za neva zinapatikana kwa karibu kila mtu. Wanasayansi wengine wanaamini kuwa hii ni tabia ya asili iliyokua kwa binadamu, kama ilivyo kwa samaki na mamalia wengine.
Hata hivyo, watu wengine huwa na uwezekano mkubwa wa kuchochea mwitikio huu bila kujitambua. Vasovagal syncope huathiri takriban asilimia 20-40 ya watu. Kwa baadhi ya watu, inaweza kuwa kuna tatizo la moyo lililojificha.
Si jambo la kushangaza kutopata sababu maalum ya tukio la kuzimia.
NINI KINAMKUTA MTU KATIKA HALI HIYO.
Pind mtu anapopatwa na vasovagal synco huwa wa katika hali hii,Neva ya vagus huchochewa kupita kiasi.,Hii husababisha kupungua kwa mapigo ya moyo na uzalishaji wa damu kutoka moyoni,mishipa ya damu huweza kupanuka (vasodilation), jambo linalopunguza shinikizo la damu na kupungua kwa damu inayoenda kwenye ubongo husababisha kizunguzungu au kuzimia.
SABABU ZA WATU KUANGUKA BAFUNI
Baadhi ya mambo yanayoweza kuchochea mwitikio wa vasovagal ni,Msongo wa mawazo (stress),hisia kali kama hofu,Kuona damu na kushituka,Kusimama ghafla na magonjwa ya moyo ❤️🩹
Ushauri:
Ikiwa mara kwa mara unazimia au unapata kizunguzungu sana, ni vyema kumwona daktari kwa uchunguzi zaidi ili kuzuia matatizo makubwa ya kiafya.