BUTONDO:NATAKA NIWEKE ALAMA KISHAPU
Awasisitiza wananchi wajiandae na Uchaguzi Mkuu 2025
Na Marco Maduhu,KISHAPU
MBUNGE wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, amesema yeye uongozi wake ni wa vitendo wala siyo maneno, sababu anataka kuibadilisha Kishapu kupiga hatua kubwa kimaendeleo na kuweka Alama.
Amesewasisitiza pia wananchi wajiandae kushiriki kwenye uchaguzi Mkuu 2025 sababu utakuwepo kama kawaida na ni takwa la Kikatiba.
Amebainisha hayo jana Mei 26,2025 wakati akizungumza na wananchi wa Lagana kwenye Mkutano wa hadhara.
Amesema katika uongozi wake,hawezi kuwa Mbunge wa maneno, bali yeye anafanya vitendo tu, ili kuibadilisha Kishapu kimaendeleo na kuweka Alama, na kwamba tangu awe Mbunge wa Jimbo hilo tangu mwaka 2020 miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa.
“Uongozi ni vitendo wala siyo maneno, nataka niweke alama Kishapu, nitaibadilisha kimaendeleo, mfano kipindi naingia kwenye Ubunge, nilikuta Kata 3 tu ndiyo zina maji, lakini leo Kata 11 zina Maji tena ya Ziwa Victoria, na nyingine 8 zina maji ya visima virefu na bado kuna miradi inaendelea kutekelezwa,”amesema Butondo.
Kwa upande wa huduma ya umeme kulikuwa na Vijiji 48 tu, lakini sasa hivi vijiji 117 zina umeme na sasa wanakwenda kupeleka umeme ngazi ya vitongoji.
Amezungumzia pia huduma za Afya, kwamba kulika na Vituo vya Afya Vinne, yeye ameongeza Vitano na kufika Vituo 9,pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa madawa unakuwepo muda wote na vifaa Tiba.
Upande wa elimu amesema wajenga shule mpya tatu zenye thamani ya sh.milioni 620 kwa kila moja, pamoja na uwepo wa madawati.
kwa upande wa miundombinu ya barabara kwamba mwaka 2021 kulikwa na Kilomita 675 za mtandao wa barabara,lakini sasa hivi zimefika kilomita 1001.
Aidha,amesema yeye yupo kwa ajili ya maslahi ya wananchi, pamoja na kutatua changamoto zao, na kwamba hata Bungeni amekuwa wakiwasemea sana wananchi, na hivi karibuni aliwasemea juu ya zao la pamba ikiwamo kuimarisha bei na upatikanani wa Pembe Jeo na viatilifu kwa wakati.
Katika hatua nyingine Butondo,amewataka wananchi kwamba wajiandae na uchaguzi mkuu 2025 sababu utakuwepo kwa mujibu wa Katiba na kuwataka wapuuze maneno ya No Refoms No Election, sababu mabadiliko wanayotaka tayari yalishafanyiwa kazi, ikiwamo kuundwa kwa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)pamoja na Wakurugenzi kuondolewa kutokuwa wasimamizi tena wa uchaguzi.
TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza na wananchi wa Lagana kwenye Mkutano wa hadhara.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464