` NIMEPONYWA KWA UGONJWA ULIONITESA KWA MIAKA 04

NIMEPONYWA KWA UGONJWA ULIONITESA KWA MIAKA 04

 


Nilivyoponywa Baada ya Miaka Nne ya Maumivu Kupitia Kufunga na Kuomba 

Kwa takribani miaka minne,Mimi Amos Jeremia Kanyamibwa, Mkazi wa mtaa wa Kawawa, Kata ya Rusimbi, Manispaa ya Kigoma-Ujiji, niliteseka na maumivu makali katika sehemu mbalimbali za mwili wangu. Polepole, maumivu yalizidi kuwa makali kiasi kwamba sikuweza tena kutoka nyumbani hata kwa basi wala teksi. Hivyo, nilikaa nyumbani siku zote nikiwa nimekata tamaa kabisa.

Nilikwenda hospitali kwa ajili ya vipimo, na nilipopewa majibu niliambiwa nina uvimbe kwenye viungo pamoja na matatizo ya tumbo na ini. Niliendelea na matibabu kwa shinikizo la familia yangu, lakini hayakuleta mabadiliko yoyote katika hali yangu.

Hatimaye, nilipelekwa katika hospitali Bugando  jiji la Mwanza,  lakini madaktari hawakuweza kunisaidia kwa lolote. Hali yangu iliendelea kuwa mbaya zaidi. Mwisho nikafikiri labda nikijaribu kwenda hospitali kubwa Muhimbili, ningeweza kupata msaada. 

Mwezi Juni 2023, niliingia Hospitali ya wakorea jijini Dar, lakini bado hali ilikuwa ile ile—nilizidi kuwa mbaya. Nilihisi kukata tamaa kabisa, nikatoka hospitali na kurudi nyumbani.

Nilipofika nyumbani, nilijikuta nimejifungia katika huzuni kuu. Sikutaka kumuona mtu yeyote, si familia wala majirani. Nilikuwa tayari nimetumia dawa nyingi nzuri na nimetibiwa katika hospitali bora, lakini hali yangu ilizidi kuwa mbaya.

Mwezi  Januari 2024, nilisikia kuhusu Maombi Kupiganiwa na madhabahu -katika Kanisa la IEAGT-Kambi ya waebrania kwa njia ya mitandao, mahali ambapo watu hupokea uponyaji wa magonjwa mbalimbali kupitia kufunga na kuomba

Niliposikia hayo, moyo wangu ulijaa furaha kwani kulikuwa na tumaini! Sikusubiri—nikachukua biblia yangu na kitabu cha nyimbo, nikuanza kufatilia maombi na kuunganishwa na timu ya  maombi na kuanza kufunga na kuomba kwa siku 07 kwa kushirikisha wanafamilia wangu 05 na tulipatiwa maandiko maalum ya kusimamia kwa muda wote na Mchungaji wa kanisa hilo (David Mabushi)

1. Yoeli 2:12

Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, kwa kufunga, kwa kilio na kwa maombolezo.”

                                                              Isaya 58:6

“Je, si huu ndio kufunga nilikokuchagua: kufungua vifungo vya uovu, kulegeza mafungo ya nira, kuwaacha huru waliodhulumiwa, na kuvunja kila nira?”

Warumi 12:12

“Furahini katika tumaini, vumilieni katika dhiki, kusudieni kuwa na bidii katika kuomba.”

                                                           Zaburi 126:5-6

Wapandao kwa machozi, watavuna kwa furaha. Yeye atokaye huku akilia, akichukua mbegu azipandazo, atarudi kwa furaha, akichukua miganda yake.”

Niliweka utaratibu kufunga kwa masaa 6 kwa siku kwa mie pekee yangu na masaa 12 kwa wanafamilia wote na  Mungu aliniponya! 

Nilijawa na shukrani kwa rehema za Kristo, nikaendelea kufunga na kuomba. Halafu nikajazwa na Roho Mtakatifu. Ah, namshukuru sana kwa neema Yake! Sasa naruka kwa furaha na kutembea kwa furaha tele.

Hata baada ya uponyaji huo,Mchungaji David Mabushi alinisaidia kunipa mistari ya biblia ya kusimamia katika hali ya kushukuru zaidi ilioendelea kuleta ukuu ndani ya nafsi na mwili wangu wote.Mistari niliyosimamia ni hii.

Zaburi 30:11-12

“Umegeuza maombolezo yangu kuwa dansi; Umenivua nguo za gunia, ukanivika furaha; Ili moyo wangu upate kukuimbia, wala usinyamaze. Ee Bwana, Mungu wangu, nitakushukuru milele.”

                                                              Isaya 61:10

“Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki..

Habakuki 3:18-19

“Lakini mimi nitafurahi katika Bwana, nitaushangilia wokovu wa Mungu wangu. Bwana MUNGU ndiye nguvu zangu, hufanya miguu yangu kuwa kama ya paa, na kunifanya niende juu ya mahali pa juu.”

Nehemia 8:10

“...Furahieni, maana furaha ya Bwana ni nguvu yenu.”

Naishukuru madhabahu ya Kanisa la IEAGT-Kambi ya waebrania kwa uponyaji .

Jina la Yesu kristo na lisifiwe milele!

Links za kufatilia mahubiri ya kanisa la IEAGT-kambi ya Waebrania.Tazama hapa chini.

                                                  YOUTUBE:
www.youtube.com/@ieagtkambiyawaebraniachurch


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464