` STAND UNITED WANAITAKA LIGI KUU,WAICHAPA GEITA GOLD BAO 2-0 UWANJA WA CCM KAMBARAGE

STAND UNITED WANAITAKA LIGI KUU,WAICHAPA GEITA GOLD BAO 2-0 UWANJA WA CCM KAMBARAGE


Stand United wanaitaka Ligi kuu wameibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Geita Gold

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

TIMU ya Stand United wameibuka na ushindi wa goli 2-0, dhidi ya Geita Gold katika ligi ya Championship.

Mechi hiyo imechezwa leo Mei 29,2025 katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Goli la kwanza la Stand United limefungwa na Yusuph Adam dk ya 14 kipindi cha kwanza, ambapo kipindi cha pili Stand United waliongeza Goli la pili kwa mkwaju wa Penati, Goli liliofungwa na Omary Rajabu dk 85.

Baada ya ushindi huo ambapo Mechi ilikuwa ya Playoff,Stand United inasubili watakao shuka kwenye Ligi kuu,Timu ya nafasi ya 13 na 14 ambapo Mmoja atakaye shinda ndipo atacheza na Stand United ili kufuzu rasmi kucheza Ligi kuu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464