DC MASINDI AONYA WATENDAJI WANAOZEMBEA KUSIMAMIA SUALA LA LISHE


Mwenyekiti kamati ya lishe na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akizungumza Kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji wa afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na vijiji robo ya tatu Januari-Machi mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Mei 8,2025
 Mwenyekiti kamati ya lishe na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akizungumza Kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji wa afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na vijiji robo ya tatu Januari-Machi mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Mei 8,2025
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungumza kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji wa afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na vijiji robo ya tatu Januari-Machi mwaka wa fedha 2024/2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Mei 8,2025.
Na Sumai Salum  - Kishapu

Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambae pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi amewahimiza watendaji wa Kata tisa kusimamia kwa nguvu suala la lishe kwenye maeneo yao.

Ameyasema hayo Mei 9,2025 kwenye kikao cha kujadili Taarifa za utekelezaji wa afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na Vijiji kwa kipindi cha robo ya tatu Januari-Machi mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo. 

"Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha robo ya tatu Januari-Machi idara ya Afya,Ustawi wa jamii na Lishe inaonesha  Kata 20 zimejitahidi kufanya vizuri kwenu Kata tisa Itilima,Mwamashele,Mwadui Lohumbo,Sekebugolo,Bupigi,Bubiki,Kishapu,Uchunga na Bunambiyu ninataka Watendaji mkafanye kazi kwelikweli huku mkifuata sheria,kanuni,taratibu na miongozo ya kazi zenu na mashule yote Wanywe uji na chakula karne hii hatuhitaji kusikia uwepo wa utapiamulo"Amesema Masindi.

Ameongeza kuwa suala la lishe ni nyeti na muhimu hivyo kila mmoja anawajibu wa kufahamu watoto  walacho kwani ndivyo vinasababisha aishi akiwa na uelewa na upembuzi mzuri wa mambo endapo akila  chochote hata athirika peke yake bali taifa linaathirika pia.

Masindi amewakumbusha watumishi Kishapu kutumia fursa ya ongezeko la mshahara wa Rais wa Awamu ya sita Mhe.Dkt  Samia Suluhu ya 35.1% kwa  uwekezaji mitambo ya kuongeza virutibishi Kwenye vyakula ili jamii ijufunze na wao kujiongezea kipato kutokana na kutokuwepo na mitambo hiyo Wilaya humo. 

Sambamba na hayo amekabidhi zawadi ya fedha taslimu kwa waliofanya vizuri iliyoandaliwa na afisa lishe kuelekea kwa  Diwani,Mtendaji na afisa afya ngazi ya jamii Kata ya Masanga,Mkuu wa Shule ya Sekondari Ijimijya pamoja na Mtendaji wa Kata ya Shagihilu kwa kazi kubwa waliyofanya  baadhi wakitoa fedha zao,muda nje ya kazi na wanafunzi kupata chakula wawapo shuleni.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Emmanuel Johnson amewataka watendaji wa Kata  kutia bidii zaidi katika kutoa elimu, kufuatiliaji na kuhamasishaji jamii kuzingatia lishe Bora.

Afisa lishe Wilayani humo Hadija Ahmed Nchakwi ameipongeza serikali kwa juhudi mbalimbali wanazoonesha kukabiliana na kuondoa udumavu kwenye jamii kwa watoto wa mwezi 0-59 na wajawazito kwani jamii sasa imeongeza uelewa kulinganishwa na kipindi cha robo iliyopita licha ya kuwa changamoto zinatokana na viashiria mbalimbali ikiwemo kukosekana chakula mashuleni na kutotekeleza maadhimisho ya siku ya afya na lishe ngazi ya Vijiji.

"Tutaendelea kutia bidii na juhudi kubwa kuhakikisha jamii yetu inabadilika na kuondokana na kuishi kwa mazoea lakini pia niwashukuru mdau wetu  anatusaidia kutoa  elimu,vitu na fedha kuifikia jamii ambao Word  Vision wenye miradi miwili Nourish project Kata ya Lagana,Mwamashele na Ngofila pamoja na Grow project wakishirikiana na Kivulini Kata ya  Mwakipoya,Shagihilu na Somagedi" ameongeza Afisa lishe.

Mtendaji wa Kata ya Itilima Masembe Masoso kwa niaba ya watendaji tisa ambao bado wako chini suala la lishe amesema mbali na kuongoza jamii isiyokubari mabadiriko chanya wataendelea kuishauri na kuielelimisha wafahamu umuhimu wa kuzingatia lishe bora na kuondokana na ulaji wa mazoea usio na tija.

Wilaya ya Kishapu ina jumla ya Shule za Msingi na Sekondari 168 na mpaka sasa zinazopata chakula ni jumla ya  Shule 152 sawa na asilimia 90.5%.

Ostadh Adamu Njiku akizungumza Mei,8,2025 Kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na Vijiji kipindi cha robo ya tatu Januari-Machi 2024/2025 wakati akiwasilisha taarifa ya madhehebu ya kiislamu katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Afisa kutoka Ruwasa wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Sumaiya Mohammed akizungumza Mei,8,2025 Kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na Vijiji kipindi cha robo ya tatu Januari-Machi 2024/2025 wakati akiwasilisha taarifa ya Ruwasa katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Afisa wa Tasaf Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Ibrahim Sakulla akizungumza Mei,8,2025 Kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na Vijiji kipindi cha robo ya tatu Januari-Machi 2024/2025 wakati akiwasilisha taarifa divisheni ya maendeleo ya jamii katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Afisa mifugo Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga Anna Kimati akizungumza Mei,8,2025 Kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na Vijiji kipindi cha robo ya tatu Januari-Machi 2024/2025 wakati akiwasilisha taarifa ya mifugo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Afisa kilimo mwandamizi wa Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga Robert Mhina akizungumza Mei,8,2025 Kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na Vijiji kipindi cha robo ya tatu Januari-Machi 2024/2025 wakati akiwasilisha taarifa sehemu ya kilimo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Afisa elimu ya watu wazima msingi Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga Baraka Mwijarubi akizungumza Mei,8,2025 Kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na Vijiji kipindi cha robo ya tatu Januari-Machi 2024/2025 wakati akiwasilisha taarifa divisheni ya elimu awali na msingi katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Afisa lishe Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Hadija Ahmed Nchakwi akizungumza Mei,8,2025 Kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na Vijiji kipindi cha robo ya tatu Januari-Machi 2024/2025 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya idara ya afya,ustawi wa jamii na lishe kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Afisa elimu watu wazima Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga Moshi D Moshi akizungumza Mei,8,2025 Kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji afua za lishe ngazi ya Wilaya,Kata na Vijiji kipindi cha robo ya tatu Januari-Machi 2024/2025 wakati akiwasilisha taarifa ya divisheni ya elimu sekondari katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.




Mtendaji wa Kata ya Itilima wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Masembe Masoso akizungumza namna atakavyojipanga kuibadilisha jamii yake kuongeza uelewa wa lishe Mei 8,2025 katika kikao cha kamati chakujadili taarifa za utekelezaji shughuli za lishe robo ya tatu Januari-Machi 2024/2025 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464