CCM: Mrema,G55 karibuni

MOROGORO: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinawakaribisha kujiunga na chama hicho John Mrema na wenzake kutoka katika kundi la G55 waliojiondoa katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla ameeleza hayo leo Mei 7,2025 wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Turiani Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku saba katika mkoa huo.
Makalla ameeleza hayo baada ya wajumbe wa Sekretarieti ya Chadema iliyomaliza muda wake akiwemo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Benson Kigaila, aliyekuwa Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu, Catherine Ruge na Mrema kutangaza kujiondoa katika chama hicho kuanzia leo.

Makalla amebainisha kuwa amefurahishwa na kauli ya G55 kwamba walihitaji kuondoka Chadema kwa sababu wanachama hao ndoto na haja yao ni kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Ameongeza pamoja na kundi hilo hawajaweka wazi ni chama gani ambacho wanania ya kwenda kujiunga nacho kati ya vyama 18 vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi, lakini Makalla alisema wanawakaribisha kuwa wanachama wapya wa CCM kwani wao wapo tayari kushiriki uchaguzi.
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO HABARI LEO
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464