` DC MASINDI AKUTANA NA WANANCHI DUGUSHILU, ASIKILIZA NA KUTATUA KERO NA CHANGAMOTO

DC MASINDI AKUTANA NA WANANCHI DUGUSHILU, ASIKILIZA NA KUTATUA KERO NA CHANGAMOTO

 

Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Dugushilu Kata ya Igaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Dugushilu Kata ya Igaga Mei,14,2025 katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi wa kijijini hicho.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Dugushilu Kata ya Igaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Sonda Nghang'ami akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo na wananchi wa Kijiji cha Dugushilu cha kusikiliza changamoto zao Mei,14,2025 katika viwanja vya Zahanati.
Mkaazi wa Kijiji cha Dugushilu Kata ya Igaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Kalag'ha Sangalali akizungumza kwenye mkutano wa Mkuu wa Wilaya hiyo wa kusikiliza changamoto zinazowakabili Mei,14,2025
Mkaazi wa Kijiji cha Dugushilu Kata ya Igaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Julius Joseph akizungumza kwenye mkutano huo
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Dugushilu Kata ya Igaga kwenye Mkutano wake wa hadhara wa kusikiliza changamoto zinazowakabili Mei,14,2025 katika viwanja vya Zahanati.
Mkaazi wa Kijiji cha Dugushilu Kata ya Igaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Willy Gamba akizungumza kwenye mkutano wa Mkuu wa Wilaya hiyo wa kusikiliza changamoto zinazowakabiri Mei,14,2025
Familia zilizovamiwa na mnyama aina ya fisi mnamo Desemba 12,2024 na kusababisha vifo vya watoto wawili na watu kadhaa kujeruhiwa.
Mkaazi wa Kijiji cha Dugushilu Kata ya Igaga Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mayunga Jidai akizungumza kwenye mkutano wa Mkuu wa Wilaya hiyo wa kusikiliza changamoto zinazowakabili Mei,14,2025
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga David Mashauri akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo na wananchi wa Kijiji cha Dugushilu cha kusikiliza changamoto zao Mei,14,2025 katika viwanja vya Zahanati.


Na Sumai Salum-Kishapu 

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Dugushilu kilichoko Kata ya Igaga ambapo amepokea kero na changamoto zinazowakabili wananchi wa eneo hilo.

Katika mkutano huo uliofanyika Mei,14 2025 kwenye viwanja vya Zahanati ya Kijiji hicho Mhe. Masindi amesema amefika hapo kwa lengo la kusikiliza na kushughulikia matatizo yao sambamba na kutoa salamu za pole kwa familia na waathirika wa tukio la kushambuliwa na mnyama mkali aina ya fisi mnamo Disemba  2024.

Miongoni mwa kero zilizowasilishwa na wananchi ni pamoja na ubovu wa barabara,ukosefu wa madaraja pamoja na ukosefu wa huduma za afya kwa zahanati kuchelewesha kufanya kazi.

Akijibu swali la Julias Joseph aliyehoji kuhusu ukamilishaji wa ukarabati wa barabara ya Mhunze-Dugushilu na Uchunga-Dugushilu hadi Ikonda amesema mkandalasi wa eneo hilo  alifuata vifaa vya ujenzi wa daraja na kufikia jumapili Meo 18,2025 vifaa vitakuwa eneo la ujenzi ili kazi iendelee.

Mhe. Masindi ameahidi kushirikiana na viongozi wa Halmashauri pamoja na wadau wa maendeleo kuhakikisha kuwa changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi wa haraka ili kuboresha maisha ya wananchi wa Dugushilu na kata nzima ya Igaga Igaga huduma zote za msingi ziwafikie.

Amezikumbusha familia kila mmoja kutimiza wajibu wake huku wakidumisha uwazi katika matumizi ya fedha wanazopata hasa wakitoa kipaumbele kwa kuwahudumia na kuwatunza watoto wao mahitaji yote ya msingi ususa ni elimu.

"Tumeanza rasmi msimu mpya wa pamba 2025/2026 nyie wanaume hatutaki kusikia kuhusu unyanyasaji wanawake ni waaminifu sana kwenda shamba kuhakikisha mnapata mavuno mengi sio uuze pamba na mazao mengine kisha uende mjini kutumia na wanawake wengine huku mke wa watoto wanateseka utalaaniwa na Mwenyezi Mungu hakika" ,amesema Mkuu huyo.

Ameongeza kuwa elimu inaongeza thamani ya mtu hivyo wazazi na walezi wanahitajika kuwasomesha watoto wao kwa mali zao zote na sio kuwatumikisha kwa kuchunga mifugo,kilimo na kazi za majumbani. 

"Nje na suala la elimu niseme tu Ardhi inazidi kupanda thamani kila siku na sasa Kata mbili zimeingia kwenye Mamlaka ya Mji  Mdogo Kishapu Kishapu Sisi hapo baadae Igaga mtaingia hivyo msiuze hovyo ardhi mlizonazo wekezeni miradi kwa fedha mliyonayo kisha Mungu atawainua na kuwaongeza" ameongeza Masindi.

Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani amewataka kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo kwenye maeneo yao na sio viongozi wanaotanguliza masilahi yao wenyewe.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo David Mashauri akijibu swali ya Willy Gamba kuhusu kuanza kutumika kwa zahanati hiyo amesema ifikapo mwezi juni  mwishoni wametazamia vifaa kufika na kisha itaanza kuwahudumia wananchi.

Diwani wa Kata ya Igaga Mhe.James Kamuga amesema wananchi wanashauku kubwa ya kupata huduma ya afya kwenye eneo lao hivyo watajadili kwa pamoja ili waanze ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa afya na kisha serikali iwasaidie kukamilisha kama walivyofanya kwenye ujenzi wa boma la zahanati lililoanzishwa kwa nguvu za wananchi.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464