` MISA TANZANIA YAMLILIA CHARLES HILLARY

MISA TANZANIA YAMLILIA CHARLES HILLARY

MISA TANZANIA YAMLILIA CHARLES HILLARY

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tan), imetoa salamu za pole kufuatia kifo cha mwanahabari mkongwe Charles Hillary, ikisema itaendelea kukumbuka mchango wake mkubwa katika sekta ya habari hapa nchini.

Mwenyekiti wa MISA Tan, Edwin Soko, amesema kuwa marehemu Hillary alikuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza taaluma ya habari na kutetea uhuru wa vyombo vya habari.

“Tumempoteza mtu muhimu sana katika tasnia ya habari. Charles Hillary alikuwa mfano wa kuigwa kwa wanahabari wengi kutokana na weledi, ujasiri na kujitolea kwake kwa maslahi ya taaluma,” alisema Soko.

MISA Tan imeeleza kuwa itaendelea kuenzi ujasiri wa marehemu kwenye kuipambania sekta ya habari na pia inatoa pole Kwa familia na watanzania wote
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464