


Jogoo wa jamaa atoweka baada ya kumchukua mrembo wa baa
Kutana na simulizi ya kijana mmoja, James ambaye anaamini kuwa mwanamke aliyemchukua kwenye baa usiku mmoja na kulala naye kwenye nyumba ya kulala wageni huko Kagera ndiye aliyehusika na masaibu anayopitia kwa sasa.

James yuko tambarare kabisa pale maeneo, kwa ufupi jogoo wake umetoweka, kutokana na hilo, hajaonekana nyumbani ambapo mkewe na watoto wake wawili wanangojea kwa hamu kurudi kwake.