` DR. SAMIA KATAMBI DAY YAFANA SHINYANGA,MILIONI 61 ZATOLEWA UKAMILISHAJI MIRADI

DR. SAMIA KATAMBI DAY YAFANA SHINYANGA,MILIONI 61 ZATOLEWA UKAMILISHAJI MIRADI

DR. SAMIA KATAMBI DAY YAFANA SHINYANGA,MILIONI 61 ZATOLEWA UKAMILISHAJI MIRADI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

Maadhimisho ya Dr. Samia Katambi Day yamefanyika kwa mafanikio makubwa mjini Shinyanga, yakihusisha ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwa helikopta pamoja na kufunga rasmi mashindano ya michezo ya jadi yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Patrobas Katambi.
Ziara hiyo imefanyika leo Mei 16,2025 pamoja na kuhitimishwa kwa Michezo ya Jadi na Katambi, katika viwanja vya CCM Kambarage.

Katika ziara hiyo, Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), alitoa zaidi ya Shilingi milioni 61 kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Zahanati.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza na hadhara ya wananchi, amesema siku hiyo ya Dr.Samia/Katambi Day ni yakufurahi miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa katika Jimbo la Shinyanga Mjini na Mkoa mzima.

Amesema katika miaka minne ya uongozi wa Rais.Dr Samia Suluhu Hassan,katika jimbo la Shinyanga Mjini na Mkoa mzima wa Shinyanga,fedha nyingi zimetolewa kwa ajili ya utekelezwaji wa miradi ya maendeleo.
"Leo tunasherehekea maendeleo makubwa yaliyofanywa na Rais.DR Samia Suluhu Hassan katika Jimbo la Shinyanga Mjini, kwa burudani pia ya Michezo ya Jadi,"amesema Mlolwa.

"Sisi hatuna cha kumpa Rais Dr.Samia kwa mazuri aliyoyafanya hapa Shinyanga zaidi ya kumuenzi,Shinyanga ya sasa siyo ile ya zamani imepiga hatua kubwa kimaendeleo,"ameongeza Mlolwa.
Aidha,amempongeza Mbunge Katambi kwamba aliochaguliwa na wananchi hakuwa Mbunge mzembe,bali amekuwa mtu wa kushughulikia matatizo ya wananchi na sasa matunda yameonekana ambapo miradi mingi imetekelezwa, na wao kama viongozi wa CCM wamejionea kwa macho yao.

"Tangu asubuhi tumeitembelea miradi ya maedeleo tena kwa Helkopta lakini tumeshindwa kuimaliza,ni miradi mingi sana ambayo imetekelezwa katika Jimbo hili la Shinyanga Mjini,"amesema Mlolwa.
Kwa upande wake Mbunge Katambi, ameteja miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa kuwa ni ukamilishaji wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa iliyo Mwawaza, na kwamba kwa sasa wapo kwenye mchakato wa uwekaji barabara kwa kiwango cha Lami sababu Mkandarasi ameshapatikana.

Amesema katika Sekta hiyo ya Afya,imekarabatiwa pia Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga,ujenzi wa Zahanati, Vituo vya Afya na utolewaji wa vifaa tiba vya kisasa.
Amesema, pia yamejengwa madaraja ambayo yalikuwa korofina sasa yanapitika, pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara,

Kwa upande wa elimu,amesema shule nyingi mpya zimejengwa za msingi na sekondari, ikiwamo na shule ya Wasichana iliyopo maeneo ya Butengwa.
Amesema pia imejengwa machijio mpya ya kisasa,masoko mapya na mengine yameboreshwa, na sasa wafanyabiashara wanauza bidhaa zao katika mazingira rafiki.

Pia, umeutaja ujenzi wa uwanja wa ndege wa Ibadakuli, kwamba kwa sasa umeshakamilika kwa asilimia kubwa na hata wao wameutumia leo kutua na Helkopta.
Katika hatua nyingine,amesema ataendelea kudhamini michezo ya jadi,ili kuendelea kuuenzi utamaduni wa Mwafrica.

Afisa habari wa michezo hiyo ya Jadi wilaya ya Shinyanga Eneza Kanuya,amemshukuru Mbunge Katambi kwa kuwadhamini na kuienze michezo hiyo ya Jadi.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira Vijana na watu wenye ulemavu akizungumza.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464