` DC MASINDI AKUTANA NA WANANCHI MWASUBI, AHAMASISHA KUJENGA GHALA LA KISASA

DC MASINDI AKUTANA NA WANANCHI MWASUBI, AHAMASISHA KUJENGA GHALA LA KISASA

 

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi akizungumza kwenye makabidhiano ya ghala la kihifadhia pamba ambapo Amcos ya Mwasubi watalitumia kwa muda likiwa ni mali ya wakulima wa Kata ya Bunambiyu Mei 16,2025

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi(wa kwanza kulia) akimkabidhi ufunguo wa ghala la kuhifadhia pamba kwa muda wakati wakiendelea na ujenzi wa ghala kwenye Kata yao mwenyekiti wa Amcos ya Mwasubi Gole Mashine( wa pili kutoka kwa Mkuu wa Wilaya) Mei,16 2025 wakiwa Kata ya Bunambiyu

Mkaazi wa Kijiji cha Mwasubi Juma Samwel akihoji kuhusu ukosefu wa Zahanati,maji safi na salama pamoja na ubovu wa Barabara katika mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi na wananchi wa Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi Mei 16,2025.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi (kushoto) na Mwenyekiti wa Kijiji cha Bunambiyu (kulia) Jekela Mussa wakiangalia Ghala linalotolewa kutumika kwa muda na Amcos ya Mwasubi.

Mkazi wa Kijiji cha Mwasubi Daud Lupuga akitaka kujua hatima ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata hiyo ulioshindikana kutokana na migogoro wa kijiji na kijiji alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi na wananchi wa Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi Mei 16,2025.

****

Na Sumai Salum-Kishapu

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi ameendelea na utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi kwa kufanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika huduma za kijamii.

Katika mkutano huo uliofanyika Mei 16,2025 Mhe. Masindi amesisitiza umuhimu wa kujenga ghala la kisasa kwa ajili ya kuhifadhi pamba ili kuongeza thamani na kuimarisha kilimo cha zao hilo muhimu katika eneo hilo kwa wakulima wa Kata na Kijiji hicho ambao wanakabiliwa na ukosefu wa ghala.

Ameeleza kuwa uwepo wa ghala hilo utasaidia wakulima kuhifadhi pamba kwa usalama, kuepuka hasara na kuongeza kipato.

"Natoa onyo kali kwa watu wachache wanaotishia amani na utulivu katika Kata ya Mwasubi na Bunambiyu kutokana na ugomvi wa ghala lililojengwa mwaka 1954 kabla Kata hizo hazijagawanywa serikali haitawavumilia watu wanaochochea migogoro au vurugu hivyo nyie mwasubi anzisheni ujenzi wa ghala lenu",amesema Masindi.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewakumbusha wananchi kuwa urithi wa kweli ni elimu kwa watoto wao kwani Urithi wa mali mara nyingi huleta maafa, lakini elimu ni urithi wa kudumu unaomkomboa mtu hivyo kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari serikali ya Kijiji na Kata itashirikiana na ofisi ya Mkurugenzi kuona ni wapi patafaa ili fedha walizochanga wananchi kufanyiwa kazi hiyo mara moja.

Katika hatua nyingine, aliwahimiza wananchi kuanza ujenzi wa boma la zahanati huku akiahidi kuwa serikali itahakikisha inakamilisha ujenzi huo pindi hatua za awali zitakapokamilika.

Amesisitiza kuwa maendeleo ni jukumu la kila mwananchi na si ya serikali peke yake huku
Kwa upande wa kilimo, wakulima wenye uwezo wa kifedha kununua dawa za kuua wadudu waharibifu wa pamba badala ya kusubiri msaada wa serikali.

Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya serikali na wananchi ndio njia bora ya kufanikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani humo Shija Ntelezu amewataka wananchi kusikiliza kauli za viongozi wao huku wakifanya kazi kwa bidii ili waongeze kipato cha mtu mmojammoja na Wilaya kwa ujumla.

Mkutano huo umetoa fursa kwa wananchi kueleza changamoto zao, huku wengi wakionesha matumaini makubwa juu ya hatua zinazochukuliwa na serikali ya Wilaya ya Kishapu chini ya uongozi wa Mhe. Peter Masindi.


Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Joseph Swalala akifuatilia mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya na wananchi wa Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi Wilayani humo Mei 16,2025
Mkazi wa Kijiji cha Mwasubi Salu Charles akihoji kuhusu mgogoro wa ghala kati ya Kata ya Mwasubi na Kata ya Bunambiyu pamoja na ujenzi wa shule ya Sekondari Kata ya Mwasubi.
Mkazi wa Kijiji cha Mwasubi Henry Yonzo akihoji kuhusu ucheleweshaji wa dawa ya kunyunyuzia pamba na hata ikija haitoshelezi mahitaji ya wakulima alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi na wananchi wa Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi Mei 16,2025.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwasubi Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Gesa Kija akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo cha kupokea changamoto za huduma za kijamii walizonazo Mei 16,2025 Kijijini hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi Wilayani humo Mei 16,2025 wakati akijibu changamoto za huduma za kijamii walizonazo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Shija Ntelezu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo na wananchi wa Kijiji cha Mwasubi wenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za huduma za kijamii walizonazo Mei 16,2025
Mkaazi wa Kijiji cha Mwasubi Salu Charles akihoji kuhusu hali ya wanunuzi wa pamba katika mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi na wananchi wa Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi Mei 16,2025.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Mwasubi Kata ya Mwasubi Wilayani humo Mei 16,2025 wakati akijibu changamoto za huduma za kijamii walizonazo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464