MAMENEJA SHINYANGA WAKUTANA KUJENGA USHIRIKIANO”MANAGER’S CONNECT 2025”
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MAMENEJA kutoka taasisi mbalimbali,mashirika, na makampuni,wamekutana mjini Shinyanga katika tukio maalum la Shinyanga Manager’s Connect,lenye lengo la kujenga mshikamano na kuimarisha ushirikiano baina ya sekta binafsi, serikali na jamii kwa ujumla.
Tukio hilo limefanyika jana Mei 10,2025, ambalo lililenga pia kuwa jukwaa la kushirikiana taarifa, kujadili njia bora za kuwahudumia wananchi, pamoja na kuhamasisha huduma bora kupitia majukwaa ya pamoja.
Mratibu wa tukio hilo Amos John ambaye pia ni MC Mzungu Mweusi, amesema kuwa dhamira ya kuandaa tukio hilo ilitokana na utambuzi wa mchango mkubwa wa mameneja katika kuleta maendeleo kwenye jamii kupitia huduma zao.
“Naamini kuwa tukishirikiana kama familia moja, tutaweza kuleta mabadiliko chanya kwa kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na kukuza mshikamano katika jamii,”amesema Amos.
“Leo nimealika waandishi wa habari ili kutumia jioni hii kama jukwaa la kueleza huduma mnazozitoa kwa jamii. Lengo ni kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu mchango wenu,” ameongeza.
Amefafanua kwamba kupitia mkutano huo, kuna nafasi pia ya kuandaa kampeni, warsha, na matukio ya kijamii kwa kushirikiana kwa karibu zaidi na taasisi husika ili kufanikisha malengo ya pamoja.
Aidha,aliwasilisha ombi lakuendelea kushirikiana zaidi na taasisi hizo katika matukio mbalimbali ya kijamii, kisekta na kitaaluma, ikiwa ni pamoja na kampeni, matamasha, na shughuli nyingine zenye maslahi ya pamoja.
“Kwa moyo wa dhati,naomba nafasi ya kushirikiana nanyi zaidi kama MC Mzungu Mweusi,katika kampeni, matamasha na shughuli mbalimbali za taasisi zenu,”amesema Amos.
Nao baadhi ya Maneja hao wamelipokea tukio hilo kwa matumaini makubwa, ambapo wameonesha nia ya kuendeleza ushirikiano kwa manufaa ya jamii ya Mkoa wa Shinyaga.
Pamoja na mambo mengine ulifanyika pia uchaguzi wa viongozi ili kuendeleza umoja huo wa Mameneja, ambapo Joyce Chagonja Meneja wa Benk ya NBC alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, akisaidiwa na Meneja wa Benki ya NMB Gadiel Sawe,huku Katibu akiwa ni Dk.John Kasubi kutoka Cho cha Serikali za Mitaa Hombolo na Msaidizi wake ni Karembo Peter kutoka Chuo cha Madini.
Pia,alichaguliwa Mhasibu ambaye Mkuu ambaye ni Julius Mataso kutoka TCB Benki, na Msaidzi wake ni Sylivia Sylivery kutoka Gven Wear.
TAZAMA PICHA👇👇
Muandaaji wa Shinyanga Manager's Connect,Amosi John maarufu Mzungu Mweusi akizungumza.
Katibu wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Maselina Saulo akizungumza.
Mameneja wakizungumza.
Vyeti vya shukrani vikitolewa.
Viongozi wa Mameneja Shinyanga waliochanguliwa katika picha ya pamoja.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464